Wakuu, kati ufaulu wa Written interview na Oral Interview ipi Wana consider sana wakati wa placement prioritization?

So, kuwa na alama nyingi kwenye written Interview haitakuwa na msaada endapo mtahiniwa atapa alama chache kwenye Oral Interview?
 
Kwa hiyo hizo offer letter 5 bado zipo wanakusubiri uzikubali offer zao ?
Chief, namaanisha tangu nimalize chuo kikuu nilifanya interview 9(ya serikali ni 1 tu ya juzi) niliwahi kufaulu interview 5. Kwa Sasa nipo sekta binafsi
 
Nimeamka kusali, nilipomaliza nikasema nipite humu, nikaona uzi wako uko juu kabisa. Written ndiyo iliyokupitisha kuingia kwenye Oral, kwa maana hiyo kazi yake iliisha. Sasa watakupima kwenye Oral ila usikate tamaa, usiogope wala kukosa usingizi.

Lala na muachie Mungu mwenyewe, akatende kadri jinsi ulivyomuomba na jinsi atakavyopendezwa. Kutofanya vizuri kwa hayo mawili, huenda kuna wengine pia imekuwa ni zaidi yako. Tegemea tu taarifa nzuri, ondoa hofu.
 
Ahsante mkuu 🙏🏽
 
Ukifanikiwa kuingia kwenye Oral Interview, yale matokeo ya Written achana nayo kabisa juwa kwamba unaenda kwenye mpambano mwingine, cha msingi hata kama usipopata hiyo nafasi uliyoomba kwa sasa basi unatakiwa upambane upate walau alama 50 ili ubakie kwenye Data base. Endelea kumuomba Mwenyezi Mungu lolote linaweza kutokea wala usikate tamaa katika hili.
 
Duh 🙄
 
Interview panel huwa hawaangalii tu namna ya ulivyojibu swali, kuna vitu vingi wana vizingatia ikiwemo muonekano (mavazi), kujiamini n.k
Kama ni hivyo tuombe Mungu, huenda nikapata hii kazi
 
Kama ni hivyo tuombe Mungu, huenda nikapata hii kazi
Na ndio maana hata wale wasimamizi wa usahili huwa wanatoa utangulizi kabla haujaingia kwenye chumba cha mahojiano, huwa wanawaeleza interview candidates kwamba unapoulizwa swali basi jitahidi kuongea sio unaulizwa swali unakaa kimya au unasema SKIP, hapana jitahidi kuzungumza mle wanachotaka ni idea tu kuwa huyu mtu kweli anauelewa kiasi na hiki anachoulizwa, kwa hiyo usikate tamaa endelea Kuomba ndugu yangu.
 
Majibi sahihi haya hapa.
Mimi nilifanya written nikafaulu, Baada ya Oral walipotoa majina ya waliopata ile kazi sikuwepo, nikaja kupangiwa kazi nyingine miezi kama 6 baadae. Wife naye hivyo hivyo, amekuja kupangiwa baada ya miezi 3, ukifika oral tu unawekwa kwenye database.
 
Ninachokumbuka ni kwamba
1. maswali yalikuwa yanaeleweka na niliyajibu yote
2. Nilikuwa candidate wanne kuitwa kwenye panel na nilitumia muda mfupi kwenye interview kuliko walionitangulia(nilitumia kama dakika 4 tu).
3. Baada ya kumaliza, wakati nipo nje nashuka kwenye ngazi nilisikia huko ndani wakisema "wote wangekuwa kama huyu tungefunga kazi saa tisa". Sasa hii sentence ndiyo inanitia shaka kwamba je nimebornga au nimepiga?
 
Mpaka hapo jiandae kwa Placement ndugu yangu, hicho ni kiashiria kwamba yajayo yanafurahisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…