Wakuu msaada kwenye tuta: PC yangu inanyonya sana MB nini tatizo ?

Wakuu msaada kwenye tuta: PC yangu inanyonya sana MB nini tatizo ?

Bila Shaka unatumia windows 10 au 11 hizi Zina mtindo wa kuji update. Weka windows 8 na unapo install Zima automatic updates
 
Windows 10 na windows 11 ni Os ambazo kila siku Microsoft wanatoa viupdates vidogo vidogo. Kwa hiyilo ukiwa kwenye internet hizo updates lazma zitajidownload ili PC yako izidi kufanya kazi vizuri.
Kama una windows 10, angalia ni version ya mwaka gani kwaku search pale chini WINVER,. Version ya mwisho ya windowa 10 ni 22H2, sasa kama unachini ya hapo kwa mfano version inayoanzia namba 15 inamaana ya mwaka 2015, 16 inamaana ya mwaka 2016, 19 inamaana 2019 nakadhalika.
Sasa kama unayo ya mwaka 2019 kwa mfano, ukiconnect kwenye internet itakula data ikijiupdate kwenda kwenye version ya mwaka 2022 ambayo ni 22H1 au 22H2. Hapo ndipo unapona pc yako haifai.
Lakini ikifanikiwa kumaliza kujiupdate mpaka mwisho, utainjoy sana Data lako.
Kwa wale ambao pc zao zinashinda kwenye internet na wanatumia win 10, mtakubaliana na mimi kwamba kuna wakati ziliwaomba kujiupdate kwenda windows 11. Hiyo inamaanisha zilijiupdate mpaka 22H2 ya windows 10 na inahitaji vi MB kidogo tu kuingia window 11 version 22H2.
Kwa sasa windowa 11 ina version 23H2.
Ndio hayo braza
 
Pia angalia Real Time protection, km iko on pia inachangia maana ina auto update
Unatoa ushauri kama mlevi vile, sasa hiyo real time protection ungemueleza ataipata wapi la sivyo ushauri wako ni useless
 
Hiyo ni tempo solution maana PC iki restart itarudia mchezo ule ule.

Hiyo option kwangu haikuweza kuwa msaada na niliifanya kwa PC tatu tofauti.

Njia pekee ambayo ilionekana kuwa hopefully ni kuiset wifi katika metered connection

Metered connection ni njia ya utunzaji data kwa kuzuia baadhi ya apps zisiweze kupata access ya internet, na windows updates ikiwemo.

NB: huyu mtoa mada ni Gongowazi, leo tunampa msaada kunusuru vi MB vyake afu baadae anakuja kutuletea shombo kwenye jukwaa la sports.
Only Metered Connection can fix the problem ya jamaa mwenye hili tatizo..
 
Back
Top Bottom