Windows 10 na windows 11 ni Os ambazo kila siku Microsoft wanatoa viupdates vidogo vidogo. Kwa hiyilo ukiwa kwenye internet hizo updates lazma zitajidownload ili PC yako izidi kufanya kazi vizuri.
Kama una windows 10, angalia ni version ya mwaka gani kwaku search pale chini WINVER,. Version ya mwisho ya windowa 10 ni 22H2, sasa kama unachini ya hapo kwa mfano version inayoanzia namba 15 inamaana ya mwaka 2015, 16 inamaana ya mwaka 2016, 19 inamaana 2019 nakadhalika.
Sasa kama unayo ya mwaka 2019 kwa mfano, ukiconnect kwenye internet itakula data ikijiupdate kwenda kwenye version ya mwaka 2022 ambayo ni 22H1 au 22H2. Hapo ndipo unapona pc yako haifai.
Lakini ikifanikiwa kumaliza kujiupdate mpaka mwisho, utainjoy sana Data lako.
Kwa wale ambao pc zao zinashinda kwenye internet na wanatumia win 10, mtakubaliana na mimi kwamba kuna wakati ziliwaomba kujiupdate kwenda windows 11. Hiyo inamaanisha zilijiupdate mpaka 22H2 ya windows 10 na inahitaji vi MB kidogo tu kuingia window 11 version 22H2.
Kwa sasa windowa 11 ina version 23H2.
Ndio hayo braza