Mkuu hii niliwahi kuifanya pale Ekenywa, niliitumia Cash na kama unavyojua pale ni hospitali binafsi, kusafisha jino moja ni elfu 30, nilisafisha sita ya juu ambayo ndio yanaonekana nikicheka.... Efficiency yake sio kihivyo mkuu, huwa yanatakata kama tatizo ni plaque, ila kama yameathirika ya fluoride kama ya sisi watu wa Kilimanjaro na Arusha ni ngumu kuwa meupe, kwa sababu tatizo fluoride inaathiri kuanzia ndani mpaka juu, so ile rangi ya meno ni kutoka ndani, hata likwanguliwe vipi haiishi zaidi ya kuondoa enamel na kukuacha na tatizo lingine.
Labda achague ile ya kuvalisha meno cape flani hivi(madaktari wa kinywa wanajua kitaalamu inaitwaje) mimi nilishauriwa kufanya hivyo gharama zikanishinda. Ni ghali mnoo,ila kama mdau mfuko wake uko vizuri aende hospitali yeyote yenye huduma ya kinywa na meno watampa gharama na watamfanyia vizuri