Wakuu, nimekuta mil 300 kwenye Bank account yangu - sizijui!

Wakuu, nimekuta mil 300 kwenye Bank account yangu - sizijui!

Serikali haijalala kihivyo... akikaa kimya na wakati wa kuifuatilia ikaja onekana akaunti yake ina pesa ambayo mzunguko wake ndio huo wa haramu... Lazima ajumuishwe kwenye wizi... Maana atakuwa hana ushahidi wa kutohusika
Hatimae Benki itagundua makosa Chief
 
Hela iliopotea njia sio rahisi kuipata hio! Hapo tegemea tu kwamba washa revert muamala na unarudi ulipotoka!

Ni kama tu wewe ukigundua umekosea kuhamisha pesa unapojiwahi kupiga voda au kuzuia muamala.
 
Mkuu ukienda polisi unaweza kupewa kesi na pesa wakaipiga wao...amini nachokwamba

Mkuu ukienda polisi unaweza kupewa kesi na pesa wakaipiga wao...amini nachokwambia
ni kweli ushauri wako, naweza kufika nikapewa kesi ya utakatishaji wakati hata sijui hela imetoka wapi na inakwenda wapi
 
Hela iliopotea njia sio rahisi kuipata hio! Hapo tegemea tu kwamba washa revert muamala na unarudi ulipotoka!

Ni kama tu wewe ukigundua umekosea kuhamisha pesa unapojiwahi kupiga voda au kuzuia muamala.
Mkuu bado hela bado imo.... nimecheki tena muda huu.
 
Mi siamini hata chembe kwamba hizo pesa zimeingia kimakosa kwenye akaunti yake... Hata kidogo
Huwa zinaingia kimakosa ila huwa haichukui muda wanagundua na kama ikatokea ukaingiza ATM cadi unaewza kutoa kiasi ila kumbuka wanaweza kukufunga
 
ni kweli ushauri wako, naweza kufika nikapewa kesi ya utakatishaji wakati hata sijui hela imetoka wapi na inakwenda wapi
Isikilizie kama baaz ya wadau wanavosema kisha chomoa kidogo kidogo,kama ni haramu huwezi kutafutwa,mwizi kaiba nae kaibiwa ngoma droo
 
Naomba ushauri tu, leo nimekuta Mil 300 zimo kwenye account yangu ya Benki - Sijui zilikotoka sasa naomba ushauri kwenu je
1. Ni report bank yangu kwamba kuna mzigo sijui ulikotoka
2. Nikae kimya kwanza kusikilizia
3. Nianze kuzitumbua
4. Nizihamishe fasta kwenye acc nyingine
5. Nizitoe zote nikae nazo home, sababu wanaweza ku-trace kama nikiweka kwenye acc yangu nyingine?
........

wazoefu naombeni ushauri wenu - nimedata hata kazi nashindwa kufanya - Jina la Benki naliweka kapuni kwa sasa.
Zamani watu walikuwa wanazila tu. Cku hizi ukizila, unashtakiwa kwa uhujumu uchumi. Chukua kama laki tano tu hapo uka spend kidogo.
 
maisha haya mtu anaweza kuwa kuchaa kwaajiri ya pesa na pesa siyo zake, tayari umedata mzee baba
 
Nina uhakika 100% ingekua ni kweli ulichokiandika,ungeshapata solution pale pale

ndani ya 5 sec baada ya kuona acc inasoma hiyo amount,si kwa life hili eti mtu aone noti

njiani imedondoka aite majirani aulize nani kadondosha hiii hela wapendwa ktk bwana,No braza Not for Tanzanian...
 
Hahah wee jamaa bana ..sema Mimi nakuelewaga Sana tukiwaga pale kijiweni huwa unapenda stori za mamilioni milioni ..hahahaha eti juzi unaniambia una ndoto za utajiri wakati hapo ulipo nakujua vizuri tu huna Ata stuli. Aise Jonii unazinguaga Sana.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Dah, mkuu zali ilo usichezee utakuja kujuta maisha yako yotee, toa ela izo tenga ata 50 za kuhonga kama ikitokea shida nyingne tumia
 
Back
Top Bottom