Wakuu, nimekuta mil 300 kwenye Bank account yangu - sizijui!

Wakuu, nimekuta mil 300 kwenye Bank account yangu - sizijui!

Siyo jambo jipya kutokea hivyo kwenye akaunti za watu. Kisheria hizo pesa siyo zako na unapaswa kuripoti benki (kwa meneja wa benki). Hata hivyo unaweza ukakaa kimya kana kwamba hujui kilichotokea na wala usichukue ili uone kitakachoendelea. Kuna watu kadhaa waliwahi kuingiziwa pesa nyingi zaidi ya hizo kwenye akaunti zao na watu wasiojulikana. Baada miezi kadhaa walisakwa na kukamatwa. Sasa jamaa yangu ambaye aliingiziwa milioni zaidi ya mia nane hukuambukizwa kwa kuwa alikwisharipoti kwa meneja na hakuzichukua hadi wakati huo.
Umemaliza... Kazi imebaki kwake kuamua
 
alipewa kiasi gani Reward?au aliambulia Asante Tu
 
Kama huwezi kuzitumia kufugia kuku ili kukuza uchumi wa nchi na kutoa ajira basi " fugia ndevu"
 
Naomba ushauri tu, leo nimekuta Mil 300 zimo kwenye account yangu ya Benki - Sijui zilikotoka sasa naomba ushauri kwenu je
1. Ni report bank yangu kwamba kuna mzigo sijui ulikotoka
2. Nikae kimya kwanza kusikilizia
3. Nianze kuzitumbua
4. Nizihamishe fasta kwenye acc nyingine
5. Nizitoe zote nikae nazo home, sababu wanaweza ku-trace kama nikiweka kwenye acc yangu nyingine?
........

wazoefu naombeni ushauri wenu - nimedata hata kazi nashindwa kufanya - Jina la Benki naliweka kapuni kwa sasa.
Unatuonaje mkuu
 
Kama ni kweli na hukua usingizini kwamba unaota basi elewa kua hilo ni jambo la kawaida sana kutokea Bank. Kama usemavyo ni kweli basi ujue sio tu kwamba pesa hizo sio zako bali ni za moto. Utakapo zigusa kama ulivyosema mwenyewe kwa kuzitoa au kuzihamisha, kosa la UTAKATISHAJI linakuhusu

Ila ni suala ala muda mfupi tu kwenye ripoti za siku iwe Bank yako au huko zilipotoka watajua na watazirudisha zinapostahili. Ushauri wangu zitolee taarifa hapo tawini kwako au tawi la karibu la Bank yako ingawa naelewa Bank hawatakupa hata buku zaidi ya kukushukuru na kukuona muaminifu
Acha kumtisha mwenzako... kiingiacho kwa mtu chake

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Naomba ushauri tu, leo nimekuta Mil 300 zimo kwenye account yangu ya Benki - Sijui zilikotoka sasa naomba ushauri kwenu je
1. Ni report bank yangu kwamba kuna mzigo sijui ulikotoka
2. Nikae kimya kwanza kusikilizia
3. Nianze kuzitumbua
4. Nizihamishe fasta kwenye acc nyingine
5. Nizitoe zote nikae nazo home, sababu wanaweza ku-trace kama nikiweka kwenye acc yangu nyingine?
........

wazoefu naombeni ushauri wenu - nimedata hata kazi nashindwa kufanya - Jina la Benki naliweka kapuni kwa sasa.
hiyo ndoto usipoangalia utakojoa kitandani. amka
 
Yes, kuna mdau pia kanitonya hivyo kwamba ikifika mwisho wa siku leo wanaweza kuzitoa - ndiyo maana nataka nikazitoe kabla ya siku kuisha... Kuna mdau kasema kwamba nijilipue - kufa ni mbele kwa mbele ila nasita -sita roho inagoma.
Wataarifu bank yako hiyo.
Uaminifu ni kitu kikubwa sana.
 
Inawezekana ni kweli. Maana mimi liliwahi kuokota pesa ndani ya bank, na niliweka uzi kabisa hapa. Ilikuwa hivi. Niliingia ndani ya moja bank crdb mkoani morogoro, nilipoingia tu pale chini nikaona pesa tsh 13000, na ndani kulikuwa na watu wengi tu. Hii inaonyesha kabisa kwamba waliziona ila waliogopa kuziokota. Mimi nikaziokota nikaweka kwwnye mfuko wa shati. Nikaenda kuandika slip maana nilienda kutoa pesa. Watu walibaki kuniangalia tu. Nilipodraw mzigo nikasepa zangu.

Japo jamaa anaweza akawa kavuta ganja lakini mistake hizi zinatokeaga sana
 
Yes, kuna mdau pia kanitonya hivyo kwamba ikifika mwisho wa siku leo wanaweza kuzitoa - ndiyo maana nataka nikazitoe kabla ya siku kuisha... Kuna mdau kasema kwamba nijilipue - kufa ni mbele kwa mbele ila nasita -sita roho inagoma.
Huwezi toa fedha bank zaidi ya million moja kwa ATM au Mobile money....labda uingie ndani benki...na ukiingia benk kama ndo magumashi unakamatwa...kajisalimishe tu
 
Nenda karipot polisi kisha benki ili uondokane na kadhia itakayokupata baadae... Raha ya pesa utafute zako za halal
Achana na huu ushauri wa kibwege huu. Wewe hujaenda kuiba,zimekufuata. Ukienda polisi utapigiwa vibao,na nauli ya kurudia home. Huku wenyewe wakicheck namna ya kuichomoa
 
Back
Top Bottom