Wakuu nimepata Tashtwiti kuwauliza jambo hili kuhusu hawa Wachina. I smell something fishy in the future

The biggest threat ni wahindi. Kwenye Kila sekta jamaa wapi, wauzaji wakubwa wa Dawa za Binadamu (Pharmaceuticals) ni wahindi, biashara nyingi sana Kariakoo wao ndio wamiliki, mpka viwanda vya juice kama jambo, biscuit na kadhalika. They are the real threat. Posta jioni wanejaa kama vile wapo Mumbai.
 
Apartheid at it's finest. Wahindi huwa wanalaumiwa kwa kuwa hawajichanganyi na wazawa, Wazungu husifiwa kwa kujichanganya na kuoleana je kwa nini Wachina wabaguliwe kwa ku-adopt mila na tamaduni wanamoishi?
Kwa sisi ambao tunaganga njaa katika nchi za watu weupe we know how it feels pale unapobaguliwa, hii dunia imekuwa kijiji hivyo tuache uoaga kama watu hawavunji sheria na wapo TZ kihalali ni vizuri wasipojibagua nasi pia tusiwabague.
Tanganyika kuna uoga mwingi kwa kuwa wengi hawana exposure lakini Zanzibar wageni wanafurahiwa na ndiyo wenye mchango mkubwa kwa maendeleo.
 
Acha kushangaa hao ni marafiki WETU wa siku nyingi. Kama wewe ni mwanaume tongoza oa wazalishe update mtoto hybridi mwenye uwezo wa kufikiri haraka kama wachina tofauti na sisi tunawaza NGOMA na sherehe na vkoba tu bila kufanya kazi
 
Waaacheni wazaane tu, hao wakiwepo matatizo madogo madogo kama kuenea kwa chura, mende ,mijusi, panya, nyokq na mijibwa kutaisha kabisa
 
Wapo kila kona ya nchi na wanaplay low profile.. Wako kwa ground Sana..misheni yao ni ndefu sana
 
Waje tu ili wachangamshe akili zetu,kama wamekidhi vigezo kisheria,si wacguzi kwa nini tusiwakaribishe?
 
naona kwenye video nyingi huko mtandaoni kwamba china ndo nchi yenye uhaba wa ajira kuliko zote duniani, vijana wanateseka na maisha

labda wanaamini huku africa kuna uafadhali

na siku hizi wengi wanazuiliwa kuingia marekani kwasababu ni wengi sana na wanazidi idadi maalum(quotas)

najaribu kuwaza tu
 
Upo sawa kabisa mkuu. Hata mi nasema muhimu watii sheria na taratibu zetu zote
 
Hapa JF kuna wachina kibao wanatumia ID fake kutetea maslahi ya China. Ndio maana wameondoa sheria ya kuzaa mtoto mmoja maana wandgundua free space huku Africa.
 

Global citizenship

Miaka ijayo kutakuwa na global citizens. Yeyote ataweza kuishi popote, muda wowote, bila kuzuiwa na mipaka ya aina yoyote (boarderless world) Dunia ni moja na binadamu ni wamoja. Wenzetu wako fasta, wameshaanza kujiweka vizuri, sisi bado tumelala.
 
Hata China wabongo wapo wengi tu na wanaongea kichina kabisa. Dunia ya leo mtu anaishi popote pale. Tatizo lenu mlijazwa ujinga kwamba nyie mna mali sana kila mtu anawaonea wivu wakati mpo kwenye dimbwi la umaskini. TZ haina fursa kuliko China au nchi zingine.
 
Hawa jamaa tusiwachukie wala kuwaona kama ni wezi au wanyonyaji.

1.Cha msingi tuangalie tu sheria na sera zetu zinasemaje kuhusu foreigner.
2.Sheria zetu ziwe nzuri na madhubuti kulinda rasilimali za nchi.
3.Sheria ziwe kali dhidi ya wajunjaji wa sheria za nchi.
Tusiwe na negative perceptions tumuonapo foreigner,hii pia ni fursa kwa indigenous coz you can learn and make connections.

Brain drain kwa sasa haiepukiki so let's we go with it.
 
Na haya mawazo ndio sahihi kabisa na inapaswa tuishi nayo haya. Muhimu wazingatie sheria na taratibu
 
Kwani Watanzania hawapo China? Wamejazana tele, wewe endelea kusinzia ndani ya Nyehunge dunia kwa sasa ni kijiji
 
Kwani Watanzania hawapo China? Wamejazana tele, wewe endelea kusinzia ndani ya Nyehunge dunia kwa sasa ni kijiji
Mkuu influx ya Watanzanja China au Ulaya haina Impact yoyote ukilinganisha na influx yao huku kwetu.
 
Mnataka muwe koloni mara ngapi mkuu?

......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…