Wakuu ukamalia sio kazi, Kila siku nawaambia, acheni kubeti!

Wakuu ukamalia sio kazi, Kila siku nawaambia, acheni kubeti!

Duuh sawa mkuu ngoja niendelee kupata ya vocha huku,
Screenshot_20250105_213818_Chrome.jpg


Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Kamari kweli ni mbaya ila tatizo ulikua unabet kitamaa unatia buku 5 unataka ule laki hapo lazima upigwe kipigo cha mbwa koko. Nimeona win moja hapo umetia 50k umekula laki swafi kabisa.
 
Huu uraibu nilidumbukia rasmi mwaka 2016 nikapigwa wee akili ikaja kunikaa sawa mwaka 2021 Niko nyang'anyang'a. Nikasema basi sirudi Tena huko.

Hamna tim ambayo siijui, ligi zote zipo kichwani, option zote zipo kichwani lakini vichapo kwenda mbele...

Nawashangaa sana vijana wanashupaza shingo kwamba betting ni kazi, vijana acheni ujinga huo fanyeni kazi zinazoeleweka hata kama kipato ni kidogo acheni tamaa ya kuwaza vitu vikubwa matokeo yake ndio kama hayo unajikuta hata hicho kidogo ulichonacho unakipoteza.

Tangu nijiingize huko nimepoteza pesa nyingi sana ambapo ningeifanyia kazi ningekuwa mbali sana. Nashukuru ni mwaka sasa sijatia Tena pua huko na matokeo yake nimeyaona ktk uchumi wangu. Vijana chonde chonde acheni kubeti inakufirisi uchumi, akili, hata familia Yako inaitawanya!
View attachment 3193112View attachment 3193113
Tamaa zitakuua na shukuru mungu umeacha
 
Back
Top Bottom