Wakuu unaweza kuoa mwanamke mwenye chale ?

Mwamba hizo siyo chale hizo ni mvuto. Mtoto kaona aende akajizindike ili apate ndoa. Muelimishe aache uoga wewe umempenda na uko teyari kufunga ndoa bila kurogwa.
 
Chale ziki kwake wewe zinakuathiri nini? Huo ni ulinzi kijana.
Na hongera umepata mke mwenye ulinzi wa asili, hapo kwako wanga watapaona kituo cha polisi.
 
Kwa advanced technology, chale ni kama chip anayowekewa tembo Serengeti Ili kufuatilia nyendo zake na kimmonitor,

Sasa ukidhamiria kumuoa, ni shart akubali kukana maagano ya Damu kupitia chale, maagano yanavunjwa na chale zinafutwa na kufutika.

Muhimu Imani.
 
Chale ziki kwake wewe zinakuathiri nini? Huo ni ulinzi kijana.
Na hongera umepata mke mwenye ulinzi wa asili, hapo kwako wanga watapaona kituo cha polisi.
Sasa mganga mchanja chale na mchawi mrogaji Wana mahusiano ingawa Sio direct,

Hawa boss wao, wanaripoti Kwa shetani.

Sasa akikutaka shetani, atapitia Kwa mganga kufanya atakavyo.

Tattoo, chale, chip, Hina ni kitu kile kile, matumizi na malengo ndo tofauti.
 
Huwezi kuelewa kijana, we kaaa kwa kutulia humo kwenye chale zinapakwa dawa zilizochanganywa kwa mizizi na majani ya miti.

Ni kama unavyokunywa panado.
 
C Chale hazina tàtizo, wengine ni mila na tamaduni tuu wala siyo ushirikina. Chukulia kama sigda tuu.
 
Huwezi kuelewa kijana, we kaaa kwa kutulia humo kwenye chale zinapakwa dawa zilizochanganywa kwa mizizi na majani ya miti.

Ni kama unavyokunywa panado.
Wewe ndio hujui,
Kwanini dawa inahitaji Damu imwagikayo kupitia chale?

Hilo ni agani, matibabu ya kipepo yatumiayo Damu,

Ukikiuka masharti, unafuatwa kushughulikiwa.
 
Hivi ni kweli wabongo hamjui kazi ya chale mwilini?

Chale ni ulinzi, hii nchi ina wachawi kila eneo so watu wanachanja kujilinda...

NB: kanda ya kati, magharibi, ziwa na kusini hata pwani hayo ni mambo ya kawaida kabisa...
 
sio chale hiyo ni mikwaruzo midog nimepata wakati nafanya usafi uvunguni mwa kitanda jamanii
 
Chale kwingine ni urembo kama Ntwara...
Lazima unchome nchale kila mahali...
 

Kwa hiyo unaenda kufunga NDOA unayoita TAKATIFU huku ukitarajia kumwambia mchungaji kuwa, umekuwa ukizini sana na huyo mwanamke hadi ukaona chale kiunoni?

Hata hivyo kwa mazingira ya Kiafrika hata kuweka kinga ya malaria wanachanja, degedege wanachanja, kipanda uso wanachanja..nk nk nk hivyo kwa wale wanaopenda kutumia tiba za kiasili za miti shamba, chale haziepukiki...japo siwezi kujua huyo wa kwako; si ungemuuliza?
 
Kama chale zenyewe zimejificha kwenye nguo fresh tu... Ila kama ni zile za usoni hapana 🤣🤣
 
So mchungaji ndio atakusaidia kuona yaliyosirini?

Muulize akujibu unamuogopa kumuuliza Chale zake utaweza kuhoji mambo mengine mkiwa ndoani nyie.
 
Hao wananariki ndoa, lazima warudishwe kundini kwanza... sasa baada ya hapo akija na chale mpya kipondo heavy kitamhusu sana mixer kumtimua
 
Acha uoga, chale ni kama ulivo na kovu la ndui😃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…