Wakuu wa shule wanawatesa sana walimu aisee

Sijawahi pelekeshwa niwe mkweli! Kawafuma mazoba
 
Yaani Kuna shule Mkuu wa hiyo shule anawachukulia walimu wake kama watoto. Kufika kazini ni saa 1 kamili, kutoka ni saa 11 jioni na ni mkali balaa kuwaandikisha barua kila wakati.
Acha mwl mkuu achape kazi. Maendeleo ya nchi hayaji kilegelege 😃😃😃😃😃
 
Nyie Walimu mbona kila sehemu hampumui? Mbona mnaburuzwa kila kona mbona mmekubali kila mtu kufanyia mifano na mafunzo ya jambo lolote kwenu? Mnashida gani?
Aiseee😂😂😂😂😂
 
Yaani Kuna shule Mkuu wa hiyo shule anawachukulia walimu wake kama watoto. Kufika kazini ni saa 1 kamili, kutoka ni saa 11 jioni na ni mkali balaa kuwaandikisha barua kila wakati.
Kwani unataka wafike saa nne halafu saa saba waondoke watotot wabaki tu kucheza halafu wanamaliza hata hawjui kusoma
 
Sijawahi pelekeshwa niwe mkweli! Kawafuma mazoba
hata mimi sipelekeshwi na huyo kiranja wetu kazini tuheshimianea, unakuta mkuu wa shule anakurupuka kupanga kazi wakati wa likizo za wanafunzi ili apate sifa wilayani kuwa walimu wake wanafundisha mpaka likizo za wanafunzi. Huwa sifuati sifa za kijinga nafuata azimio langu langu la kazi linaniongoza vipi kwa muhula wote
 
Kuna mkuu mmoja wa shule kwa upuuzi wake aliigawa staff pande mbili akidhani anatumia devide and rule kumbe anaharibu. Tulimsusia chakula cha staff awe anakula na vibaraka wake. Alinyooka ikabidi aweke maridhiano staff iwe moja
 
Waalimu wakuu wengi ni hovyo na malofa kbs, hasa baada ya kuongezewa posho ya madaraka basi wamejiona miungu watu juu ya walimu wenzao ilhali wengi wao ni vilaza wasiojua hata nini maana ya uongozi, wanadhani kufokea walimu wenzao ndio uongozi, nanyi waalimu jitambueni basi! unafokewaje kama juha na wewe umeinama tu ?
 
Yaani Kuna shule Mkuu wa hiyo shule anawachukulia walimu wake kama watoto. Kufika kazini ni saa 1 kamili, kutoka ni saa 11 jioni na ni mkali balaa kuwaandikisha barua kila wakati.
Waalimu wa nchi hii ni viumbe wa ajabu sana, yaani miongoni mwa kundi nyonge la waalimu kwa ujumla wao, bado kuna wengine humo wanajiona bora kuliko wenzao! hili ni jambo la ajabu na la kuhuzunisha sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…