Wakuu wa shule wanawatesa sana walimu aisee

Wakuu wa shule wanawatesa sana walimu aisee

Uyo mkuu wa shule hajielewi kabisa, mkuu na walimu wote ni waajiliwa wa selikari.
Mkuu wa shule ana tabia za kinyampara
 
Yaani Kuna shule Mkuu wa hiyo shule anawachukulia walimu wake kama watoto. Kufika kazini ni saa 1 kamili, kutoka ni saa 11 jioni na ni mkali balaa kuwaandikisha barua kila wakati.
Kwaki kanuni za kazi zinasemaje?
 
Yaani Kuna shule Mkuu wa hiyo shule anawachukulia walimu wake kama watoto. Kufika kazini ni saa 1 kamili, kutoka ni saa 11 jioni na ni mkali balaa kuwaandikisha barua kila wakati.
Muda wa kutoka kazini kwa mujibu wa sheria ni saa 9:30 kama hakuna ombi la kuongeza muda wa kazi lililo kubaliwa, muda wa kufanya kazi ni masaa 9 kwa siku, sasa hiyo ya saa 11 anawalipa overtime?
 
Acha mwl mkuu achape kazi. Maendeleo ya nchi hayaji kilegelege 😃😃😃😃😃
Kuchapa kazi sio kukikuka haki za wengine ndiyo maana kuna sheria za kazi, na tatizo wakuu wa shule kama hao ndio vinara wa kuhonga maofisa wa wilaya ili walimu wasio wataka wahamishwe vituo vya kazi
 
swala la elimu sio lelemama nampongeza mkuu huyo wa shule.

hawa walimu ukileta nao usela shule inageuka mtambo wa daraja sifuri
Majukumu yote ya kazi za umma yapo kwa mujibu wa sheria na sio kwa utashi wa mtu binafsi elewa hilo ,achukue hatua kwa wale wanao kiuka taratibu lakini sio kutaa sifa yeye huku akiwaumiza wengine
 
Yaani Kuna shule Mkuu wa hiyo shule anawachukulia walimu wake kama watoto. Kufika kazini ni saa 1 kamili, kutoka ni saa 11 jioni na ni mkali balaa kuwaandikisha barua kila wakati.
Kwani ni shule ya private ao walimu hawasomi labour laws
 
Walimu wakuu wa namna hiyo hawajakutana na na walimu wanaojitambua. Hao walimu wanaoburuzwa hivyo na mkuu wao hawajitambui ni kama misukule, watamuogopaje muajiriwa mwenzao ambaye hajawaajiri na yeye kaajiriwa. Huo ukuu wa shule ni kama ukiranja tu. Walimu wakuu wa namna hiyo wana kiherehere na kujipendekeza kwa viongozi wa ngazi za juu wilayani. Uongozi ni dhamana waache kutesa walimu wenzao
Walimu wakuu ni mamlaka ya nidhamu, walimu wateja wao ni wanafunzi ambao wanafika saa 12, mpaka saa 1 uwe hujafika! Unataka kuondoka kabla wanafunzi hawajatoka!
 
Walimu wakuu ni mamlaka ya nidhamu, walimu wateja wao ni wanafunzi ambao wanafika saa 12, mpaka saa 1 uwe hujafika! Unataka kuondoka kabla wanafunzi hawajatoka!
Muda wa kufika kazini ji saa 1:30 asubuhi na kuondoka ni saa 9:30 alasiri na si zaidi ya hapo, isipo kuwa kwa makubaliano maalum ambayo yana malipo ndani yake
 
Hiki kimetengeneza umaskini sana kwa Hawa watumishi,maana unatoka mdaa ambao Huna kitu Cha kufanya kingine kukuingizia kipato.
 
Walimu wakuu ni mamlaka ya nidhamu, walimu wateja wao ni wanafunzi ambao wanafika saa 12, mpaka saa 1 uwe hujafika! Unataka kuondoka kabla wanafunzi hawajatoka!
Muda wa kuondoka Ni saa 9:30 alasiri. Saa 11 Ni kiherehere na kujikomba kwa wakubwa. Period.
 
Walimu wakuu ni mamlaka ya nidhamu, walimu wateja wao ni wanafunzi ambao wanafika saa 12, mpaka saa 1 uwe hujafika! Unataka kuondoka kabla wanafunzi hawajatoka!
wale ni kama viraja tu, hawana mamlaka ya kuburuza walimu wao kazini, tena tuko sawa kielimu au tumewapita
 
Yaani Kuna shule Mkuu wa hiyo shule anawachukulia walimu wake kama watoto. Kufika kazini ni saa 1 kamili, kutoka ni saa 11 jioni na ni mkali balaa kuwaandikisha barua kila wakati.
Poleni sana.
Hadi likizo hii mnaenda? 😀
Ualimu ni wito
 
Kumekuwa na visa vingi wakuu wa shule kunyanyasa walimu wenzao wasiojitambua. Ni wakuu wa wachache ndio hupokea vipigo pale wanapozidisha unyanyasaji. Kuna mwalimu mkuu mmoja wa kike alizabwa makofi na mwanamke mwenzake ofisini. Dada wa watu akapewa adhabu ya kupelekwa shule mbaya kijijini ndani akasote huko na afisa elimu mnoko. Visa ni vingi mara mapenzi, mara wivu wa maendeleo. Wengine ukifundisha vizuri wanafunzi wakakusifu mkuu wa shule na jopo lake wanaona wivu wanaanza kukunyanyasa kila angle ili tu kukughasi
Uko sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom