Mkuu Maalim
Mohamed Said, japo siamini kama kuna watu wowote wanaoumizwa na majina ya Kiislamu katika historia ya TANU, kitu ambacho baadhi yetu hatukubaliani na wewe ni ku blend urongo na ukweli katika baadhi ya hoja zako, kwa mfano hakuna ubishi kuhusu mchango wa Waislamu katika kupigania uhuru wa Tanganyika, ila kuna siku ukaleta urongo wa mchana kweupe kuwa chama cha TANU ni cha Kiislamu, tulikutakalia humu, Chama cha TANU kilitokana na TAA, na AA, Kiongozi mwanzilishi wa AA ni Mkiristo Mkatoliki, Cecil Matola, Kiongozi mwanzilishi wa AA ni Mkristo Mkatoliki Dr. Vedastus Kyaruzi, Kiongozi mwanzilishi wa TANU ni Mkristo Mkatoliki, Mwal. Julius Kambarage Nyerere, hakuna Muislamu yeyote ni mwenyekiti muanzilishi wa AA,TAA wala TANU, hivyo kuita TANU chama cha Kiislamu ni urongo wa mchana kweupe!.
Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga
Urongo mwingine mkubwa na mbaya ni kuhusu asilimia ya Waislamu Bungeni, ulisema ni asilimia 6% nikakukatalia kuwa ni urongo!.
Ila kwenye kipaji cha masimulizi na uwezo wa kuandika historia, kwenye jukwaa hili huna mpinzani wala mshindani, na hili nimewaeleza wazi watu humu
Kwa Simulizi za Mwana JF, Maalim Mohammed Said, Sio Mtu wa Kubezwa, Mengine ni Ukweli Mchungu!, Ila Pia Sio Mtu wa Kupuuzwa!.
Mzee Pasco
Pascal...
Ungeijua historia ya Dar es Salaam katika miaka ya 1920 na kuendelea hadi uhuru ulipopatikana 1961 ungetambua kuwa Cecil Matola asingeweza kuwa Rais Muasisi wa African Association chama kilipoasisiwa 1929.
Angalia waasisi wa African Association: Kleist Abdallah Sykes, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Suleiman Majisu, Ali Said Mpima, Mzee bin Sudi, (Cecil Matola, Raikes Kusi na Rawson Watts).
Hao kwenye mabano wakiishi Misheni Kota sehemu iliyotengwa na Waingereza waishi Wakristo.
Hawa watatu katika African Association walikuwa wageni.
Hao wengine ndiyo walikuwa wenyeji wa Dar es Salaam.
Hawa wenyeji mwaka wa 1933 wakiwa viongozi wa African Association wakaunda Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislamu wa Tanganyika) ili mapambano ya Waislamu na Waingereza kuhusu dini yao yapitie Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika.
Wazee wetu walimpa Urais wa African Association Mwalimu Cecil Matola ili kujenga umoja katika jamii ya Waafrika kwani vinginevyo chama kingechukua sura ya chama cha harakati za Waislam.
Hivi ndivyo halikadhalika ilivyokuwa kwa Dr. Vedasto Kyaruzi kuchaguliwa Rais wa TAA 1950 Abdul Sykes akiwa Katibu.
1948 TAA ilibadilisha jina kwa kuongeza neno "Tanganyika."
TAA haikuasisiwa upya.
Sasa angalia wajumbe wa TAA Political Subcommittee: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Kibwana Mwapachu, Abdulwahid Kleist Sykes, (Steven Abdallah Mhando, Dr. Kyaruzi na John Rupia).
Bado unaamini Mwalimu Nyerere ndiye aliyeasisi TANU?
Ushajiuliza kwa nini haya niliyoandika hapa hayamo katika historia ya uhuru wa Tanganyika?
Hayo mengine In Shaa Allah nitayazungumza baadae kwa utulivu baada ya wasomaji kusoma utangulizi huu