Mi sijui na wala sidhani kama ni big issue. Mimi sijauliza about you bwana Mod. Niliuliza kwa ujumla sasa kama kutunukiwa ni issue samia ametunukiwa udaktari wa heshima lakini haimaanishi ana huo uwezo sheikh wangu. Ni vijimambo tu. Kama utakuwa na uwezo utaandika mambo ya msingi ya kihistoria wa wataona watacomment. Mi kabla ya kufungua uzi naangalia hata comments pia. Nmeona sehemu nyingine una comments 4 au hazizidi 10. Ndo maana sikuzifungua.
Mtu...
Unaona hakuna comment kwa kuwa wewe ni mgeni hapa.
Hujui historia yangu katika Ukumbi huu?
Waliokuwa wanadhani wanaweza kupambana na mimi katika historia ya uhuru wa Tanganyika walikuwa wanamiminika hapa kunipinga.
Walikuwa hawajapata kusikia historia ya Kleist Sykes 1929, ya wanae Abdul na Ally 1942 wala hawajasikia historia ya Sheikh Hassan bin Ameir, Schneider Abdillah Plantan, Hamza Kibwana Mwapachu 1950 kwa kuwataja wachache waliokuwa Dar es Salaam wala Ally Migeyo wa Kamachu.
Halikadhalika walikuwa hawajapata kunisikia mimi.
Walichokuwa wamefundishwa nusu Karne ni Julius Nyerere Kaunda TANU peke yake.
Mjadala ulikuwa mkali umekwenda miezi 6 mfululizo bila kusimama wachangiaji wanafikia milioni moja.
Nawaambia mimi mjukuu wa Salum Abdallah Popo muasisi wa TANU Tabora 1954, muasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) 1955 akiwa President na Kassanga Tumbo Secretary General.
Babu yangu kaongoza mgomo wa wa 1947, 1949 na 1960 uliodumu siku 82.
Mimi nawaeleza historia ya wazee wangu walivyopambana na mkoloni mimi mdogo lakini kuna ninayokumbuka mfano wa babu yangu kuwekwa kizuizini mwaka wa 1964 baada ya maasi ya Tanganyika Rifles.
Wenzangu hawana moja walijualo ila wasilotaka kusikia ni kuwa Nyerere Mikindani alikuwa analala nyumba ya Ahmed Adam, Lindi nyumba ya Ali Naliwanda, Bukoba nyumba ya Sued Kagasheki na Moshi nyumba ya Bi. Halima Selengia.
Dar es Salaam Nyerere akiishi nyumbani kwa Abdulwahid Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu baada ya kuacha kazi ya Ualimu Pugu.
Baba yangu Said Salum alimuona Nyerere kwa mara ya kwanza hapo nyumbani kwa Abdulwahid Sykes 1952 mwaka niliyozaliwa mimi.
Yapo mengi sana.
Niliwatia darasani kuwasomesha historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.
Leo wakiona uzi wangu wanakaa mbali hawausogelei.
Nina You Tube Channel huko watu wamejaa.