Walau tungepata Mtaalamu wa Historia humu ndani

Kama ni ya Uislamu hiyo tayari naifahamu nataka historia ya ujumla siyo ya dini. Wala ya Ukristo sitaki. So hapo kwangu anakuwa amekosa vigezo
Mtu...
Historia ya mchango wa Waislamu katika kupigania uhuru wa Tanganyika ilifutwa kabisa.

Historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU ikawa ni historia ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere peke yake.

Nikaandika kitabu cha Abdulwahid Kleist Sykes kitabu hiki kikabadili historia yote ya Tanganyika pamoja na historia ya Mwalimu Nyerere.

Wengi hapa JF hawakupenda kuona historia ile iliyofutwa sasa iko hadharani.
Walijaribu kunipinga hapa lakini wote niliwashinda kwani nilikuwa na ushahidi wa kila nilichoandika.

Hali ilivyo hivi sasa nyuzi zangu zinakwepwa hakuna mwenye ujasiri na uwezo wa kupinga historia hii ya wazee wangu waliounda African Association 1929, Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika 1933 na TANU 1954 kupigania uhuru wa Tanganyika.


Toleo la Nne la Kitabu Cha Abdul Sykes​
 
Bwana Mohamed Said una mengi ya kujifunza kwa watu kama MALCOM LUMUMBA ,l Pascal Mayalla Tate Mkuu etc nimewasoma. Ni waandishi wazuri wanaandika historia ambayo inaweza fundisha wengine pia kwa ujumla. Ukipata nafasi pitia nawe maandiko ya hao watu unaweza pata kitu. Ukawa na uandishi wa kuvutia na watu wengi wakakusoma na kuchangia.
 
Mtu...
Siku zote najifunza kutoka kwa wenzangu.
Wala mimi sina shida ya watu kunisoma.

Ukiingia kwenye You Tube Channel yangu utaona ukweli wa hili.


Hilo mosi.

Pili niko kama mwandishi katika Dictionary of African Biography (DAB) kamusi la volume sita linaloeleza maisha ya Waafrika mashuhuri barani Afrika.

Mimi niliombwa kuandika historia ya Kleist Sykes (1894 - 1949).

Kleist na wanae wawili Abdulwahid na Ally walitoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika kutoka 1950 na walimpokea Julius Nyerere 1952 waliondolewa majina yao pamoja na baba yao katika historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Kadi ya TANU ya Abdulwahid ni No. 3, kadi ya Ally ni No. 2 na ya Nyerere ni No. 1.
 
Mtu...
Siku zote najifunza kutoka kwa wenzangu.
Wala mimi sina shida ya watu kunisoma.

Ukiingia kwenye You Tube Channel yangu utaona ukweli wa hili.


Hilo mosi.

Pili niko kama mwandishi katika Dictionary of African Biography (DAB) kamusi la volume sita linalorleza maisha ya Waafrika mashuhuri.

​

Mimi niliombwa kuandika historia ya Kleist Sykes (1894 - 1949).

Kleist na wanae wawili Abdulwahid na Ally walitoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika na walimpokea Julius Nyerere waliondolewa majina yao pamoja na baba yao katika historia ya ukombozi wa Tanganyika.
 
Mzee Mohamed Said anajua mengi, lakini ana changamoto ya kukosa secular presentation ya historical accounts zake!
Mzee Mohamed Said anachokifanya ni kurekebisha ufahamu wa wengi kutokana na tulichojulishwa na kufundishwa kuhusu harakati za kupigania uhuru hapa Tanganyika. Wale watu wa umuhimu kwenye harakati za kupigania uhuru wameondolewa kwa makusudi, na historia yote imekuwa-focused kwa mwalimu Nyerere. Hakuna watu wanao-practise secularism kama waislamu, ila wasifanyiwe fitina.
 
Mzee Mohamed Said anajua mengi, lakini ana changamoto ya kukosa secular presentation ya historical accounts zake!
Pulchra...
Kueleza historia ya mchango wa Waislamu si suala la dini ni kama vile inavyoelezwa mchango wa Wakikuyu katika historia ya kupigania uhuru wa Kenya.

Kinachowaumizeni ni yake majina ya Kiislamu katika historia ya TANU.

Nitafute katika Cambridge Journal of African History usome wanahistoris wa sifa: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan wameandika nini kuhusu kitabu cha Abdul Sykes.

Hakuna aliyeona udini.
 
Kinachowaumizeni ni yake majina ya Kiislamu katika historia ya TANU.
Mkuu Maalim Mohamed Said, japo siamini kama kuna watu wowote wanaoumizwa na majina ya Kiislamu katika historia ya TANU, kitu ambacho baadhi yetu hatukubaliani na wewe ni ku blend urongo na ukweli katika baadhi ya hoja zako, kwa mfano hakuna ubishi kuhusu mchango wa Waislamu katika kupigania uhuru wa Tanganyika, ila kuna siku ukaleta urongo wa mchana kweupe kuwa chama cha TANU ni cha Kiislamu, tulikutakalia humu, Chama cha TANU kilitokana na TAA, na AA, Kiongozi mwanzilishi wa AA ni Mkiristo Mkatoliki, Cecil Matola, Kiongozi mwanzilishi wa AA ni Mkristo Mkatoliki Dr. Vedastus Kyaruzi, Kiongozi mwanzilishi wa TANU ni Mkristo Mkatoliki, Mwal. Julius Kambarage Nyerere, hakuna Muislamu yeyote ni mwenyekiti muanzilishi wa AA,TAA wala TANU, hivyo kuita TANU chama cha Kiislamu ni urongo wa mchana kweupe!. Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga

Urongo mwingine mkubwa na mbaya ni kuhusu asilimia ya Waislamu Bungeni, ulisema ni asilimia 6% nikakukatalia kuwa ni urongo!.

Ila kwenye kipaji cha masimulizi na uwezo wa kuandika historia, kwenye jukwaa hili huna mpinzani wala mshindani, na hili nimewaeleza wazi watu humu Kwa Simulizi za Mwana JF, Maalim Mohammed Said, Sio Mtu wa Kubezwa, Mengine ni Ukweli Mchungu!, Ila Pia Sio Mtu wa Kupuuzwa!.

Mzee Pasco
 
Pascal...
Ungeijua historia ya Dar es Salaam katika miaka ya 1920 na kuendelea hadi uhuru ulipopatikana 1961 ungetambua kuwa Cecil Matola asingeweza kuwa Rais Muasisi wa African Association chama kilipoasisiwa 1929.

Angalia waasisi wa African Association: Kleist Abdallah Sykes, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Suleiman Majisu, Ali Said Mpima, Mzee bin Sudi, (Cecil Matola, Raikes Kusi na Rawson Watts).

Hao kwenye mabano wakiishi Misheni Kota sehemu iliyotengwa na Waingereza waishi Wakristo.

Hawa watatu katika African Association walikuwa wageni.

Hao wengine ndiyo walikuwa wenyeji wa Dar es Salaam.

Hawa wenyeji mwaka wa 1933 wakiwa viongozi wa African Association wakaunda Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislamu wa Tanganyika) ili mapambano ya Waislamu na Waingereza kuhusu dini yao yapitie Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika.

Wazee wetu walimpa Urais wa African Association Mwalimu Cecil Matola ili kujenga umoja katika jamii ya Waafrika kwani vinginevyo chama kingechukua sura ya chama cha harakati za Waislam.

Hivi ndivyo halikadhalika ilivyokuwa kwa Dr. Vedasto Kyaruzi kuchaguliwa Rais wa TAA 1950 Abdul Sykes akiwa Katibu.

1948 TAA ilibadilisha jina kwa kuongeza neno "Tanganyika."

TAA haikuasisiwa upya.

Sasa angalia wajumbe wa TAA Political Subcommittee: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Kibwana Mwapachu, Abdulwahid Kleist Sykes, (Steven Abdallah Mhando, Dr. Kyaruzi na John Rupia).

Bado unaamini Mwalimu Nyerere ndiye aliyeasisi TANU?

Ushajiuliza kwa nini haya niliyoandika hapa hayamo katika historia ya uhuru wa Tanganyika?

Hayo mengine In Shaa Allah nitayazungumza baadae kwa utulivu baada ya wasomaji kusoma utangulizi huu
 
Jaribu uwe unamsoma MALCOM LUMUMBA halafu Mzee Mohamed Said siku hizi kawa YouTuber
Sijui juu ya Malcom Lumumba , lakini Mohammed Said , yeye historia anayoijua ni ya waislamu wenzake na baba zao wa Kariakoo (nafikiri akikokaa yeye) kati ya miaka ya 1940 na 1960 tu.
Na ni perspective yake ya kuwa mpinga Kristo na si zaidi ya hapo.
 
Sijui juu ya Malcom Lumumba , lakini Mohammed Said , yeye historia anayoijua ni ya waislamu wenzake na baba zao wa Kariakoo (nafikiri akikokaa yeye) kati ya miaka ya 1940 na 1960 tu.
Na ni perspective yake ya kuwa mpinga Kristo na si zaidi ya hapo.
Jidu...
Hakika naijua historia Waislamu na wazee wangu jinsi walivyopambana na ukoloni wa Wajerumani na Waingereza.

Nimeandika kitabu na kimejumuisha wote na nchi nzima waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Ila si kweli kuwa nawapinga Wakristo.
Kitabu kipi sasa mwaka wa 26 na bado wanaonipinga hawajaandika kitabu chochote katika historia hii.

Hawajaandika kwa kuwa historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Julius Nyerere imeshikana na historia ya wazee wangu.
 
Mkuu Maalim Mohamed Said , kwenye kuizungumzia historia ya Tanganyika, wewe ni tembo, mimi ni sisimizi, kuhusu AA, TAA na TANU, mimi nazungumzia viongozi wakuu waasisi na sio wanachama waanzilishi, hata kama chama kina wanachama 100, kati yao Waislamu wakawa 99, na Mkristo ni mmoja, kisha huyo Mkristo akafanywa kuwa Mwenyekiti, huwezi kusema TANU ni chama cha Kiislamu, huku Mwenyekiti mwanzilishi ni Mkristu Mkatoliki!, huu utakuwa ni urongo wa mchana kweupe, kizungungu tunaita pure white lies!. Natamani sana tufike mahali, mtu ukiongopa, urongo ukishtukiwa, uwe na the audacity ya kukubali kukosea!

Kwenye uzi huu, Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga
uongo mkubwa zaidi, ni uongo unaoandamana na data za uongo, tunaita data za kupika, pale Kwenye mahojiano yale, alipotoa data za kupika za 76% ya wabunge wa Bunge la JMT, ni Wakatoliki!,18% madhehebu mengine ya Kikristu yaliyobakia, halafu Waislamu ni just 6%!. Huu ni urongo wa kiwango cha lami mchana kweupe. Mtu huhitaji kufanya sensa ya Wabunge Waislamu kujua huu ni urongo, bila hata sensa, Wabunge wote kutoka Zanzibar ni Waislamu ambao kabla hujawajumlisha wabunge Waislamu wa bara, hao Wanzibar tuu wenyewe wanafanya theluthi moja ya Wabunge wote!. Huu ni urongo!.

Mzee Pasco
 
................. historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Julius Nyerere imeshikana na historia ya wazee wangu.
Nafikiri unakiri kile nichoandika.
Watanganyika walikuwa wamoja katika kupigania uhuru.
Sasa ukiitazama histiria kutoka katika pesrspective ya wazazi wako, waislamu, hapo ndio unaigiza ubaguzi wa kidini.
 
Au nikusimulie sababu hasa ya kuzaliwa kwa Demokrasia Ulaya (Uingereza, Ufaransa, nk) kupitia mapinduzi mbalimbali ya kisiasa?

Pata muda tujadili hii mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…