Wale ambao tunaishi na watoto wa watu na hatujapeleka hata 100 ya mahari tukutane huku

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kwann Kaka yangu Kiranga with due respect unapendaga kwenda opposite na tamaduni na dini??


Usiseme sijajibu swali Ila sijakwenda Sawa na mtazamo wako.

Mwanaume ndiye anayeoa anakuchukua MTU kutoka kwenye ukoo wake kuja kwenye ukoo wako. Mke anahama kwake anakuja kwako ndio maana wewe unalipa kamahari flani kushukuru Kwa malezi ya binti Yao.

Mkuu ulilipa mahari kiasi flani unapungukiwa nini??

Kama umempenda mwanamke utalipa tuu.

Ni ishara ya heshima.

Tujifunze kuheshimu Mila na destruri zetu.
 
Waache wakamuane juna jamaa juzi kaenda kuchumbia kaambiwa MAHARI 7M 🤣 🤣 🤣
 
Huyu mzee ananielewa sana maana kila akipata tatizo lazima anipigie tulisovu halafu sasa ni 7 nipo na binti yake na hajawahi hata siku.moja kunigusia kuhusu mahari. Nadhani ameshanielewa kila nafanya kwa familia yake na yangu
Mzee anaweza kuwa Hana shinda kabisaa au ni mzeee Kiranga ??

Tatizo mashangazi na wajomba wanataka Chao utawaambia nini??

Wewe fanya kulipa ili kuimaliza deni.

Kuna makabila usipolipa mahari watoto wanakuwa sio wakwako.
 
Mwaka wa nane huu na watoto 2 sijatoa hata mia na tunafunga ndoa soon ...

Imeisha hiyooo....ila wazee kibunda yangu wametafuna sana .
We kama mimi mwamba. nina dume mmoja na mdada nshamaliza kuzaa na mahari sina uhakika kama nitalipaga
 
Hivi naomba kuuliza hili swala la mahali ni utamadini wa wapi ukiamgalia kiundani zaidi ni kwamba unakua umemnunua mtoto wa watu na ni nani alianzisha hili swala huu sio utamadini wetu ebu fikirisha ubongo najua humu Kuna watu wazima kabisa naomba tuwekane bayana umetoa chochote kesho mmeachana unaenda kuchukua chako ikiwa umebaki na maumivu au ndio umetoa ruksa kwa mtu amfanyie chochote anachojiskia kwa mwanao maana umeomba upewe chochote nawe umepewa
 
Mzee anaweza kuwa Hana shinda kabisaa au ni mzeee Kiranga ??

Tatizo mashangazi na wajomba wanataka Chao utawaambia nini??

Wewe fanya kulipa ili kuimaliza deni.

Kuna makabila usipolipa mahari watoto wanakuwa sio wakwako.
Siishi na mtoto wa SHANGAZI ana baba yake na mama yake na hao ndio mimi nawatambua kama wazazi wake
 

Hujajibu swali, kwa sababu hujatenganisha mahari nanbeibya kumnunua mwanamke awe mke wako.

Kwa nini sitaki hoja ya dini au utamaduni?

Kwenda na tamaduni ni logical fallacy.

Inaitwa "appeal to tradition"


Kwenda na dini ni logical fallacy.

Inaitwa "appeal to authority".


Kama jambo ni zuri, lijengee hoja kutokana na uzuri wake, si kwa sababu ya utamaduni au dini.

Kwa sababu, kwenye utamaduni kuna tamaduni nyingi mbaya, za kuua watu kuwatoa sadaka, za kuonea watoto, za kukeketa wanawake.

Kwenye dini pia kuna ubaya mwingi, wa kubagua watu wa dini tofauti, wa kuruhusu utumwa, wa kukubali mambo mengi ya uongo.

Hivyo, kama unataka kuonesha uzuri wa kitu, panga hoja, onesha uzuri wake.

Usitumie hoja ya kufuata "amri kutoka juu" kwa Mungu au utamaduni.

Hiyo ni logical fallacy.
 
Mimi nimjomba wa huyu bint,yafuatayo andaa

MKAJA 200000
Uchafuzi 200000
jembe na blanket ng'ombe 3 zenye miguu minne

Mali Sasa
Milion 4

Mwaka huu usiishe kadiri miaka inavyokwenda ndivo gharama zinapanda
 
Mahari imepitwa na wakati.

Inashusha utu wa mwanamke, inamfanya mwanamke awe ananunuliwa kama ng'ombe.

Kitu muhimu watu wajenge familia tu.

Hiyo familia ya huyo mwanamke imeelewa hilo.
Ni jamii ipi hapa duniani haitoi mahari? Kila jamii inatoa mahari.

Kinachotofautiana ni kwamba, jamii moja mwanaume anamtolea mwanamke mahari, na jamii nyingine mwanamke ndiye anamtolea mwanaume mahari. Lakini sharti itolewe.

Kupinga utaratibu wa mahari ni kukwepa majukumu, iwe jamii zetu hizi ambazo wanaume wanatoa mahari au zile ambazo wanawake wanatoa mahari.

Na kama mtu anaogopa kutoa mahari, ni dhahili hata majukum mengine ya familia atayakimbia.
 
Kunyanyasa wanawake ni swala la asili. Either umelipa mahari au haujalipa mahari
 

Sijui umetembea na kukaa katika jamii ngapi mpaka umeandika ulichoandika.

Marekani hatuna mahari.

Ulaya hakuna mahari.

Kukataa mahari si kuogopa kutoa mahari. Kuna watu wanapinga mahari kwa sababu za kifalsafa.

Nyerere alikuwa mtoto wa Chifu, amesoma mpaka Ulaya zamani, kaja kuongoza nchi ya Tanzania na taasisi za kimataifa, kaongoza nchi katika vita.

Huyu si mtu muoga. Hakuogopa mahari.

Lakini ameipinga mahari kifalsafa.

"Nyerere describes bride price as evil in posthumous bio"

 
Huko kwenu marekani, familia ya mwanamke hugharimia harusi. Hiyo ndiyo mahari yenyewe. Au wewe unaelewa nini kuhusu mahari?
 
Huko kwenu marekani, familia ya mwanamke hugharimia harusi. Hiyo ndiyo mahari yenyewe. Au wewe unaelewa nini kuhusu mahari?
Kwanza, kugharimia harusi si mahari.

Pili, hata Marekani, hizo ni tamaduni zilizopitwa na wakati, siku hizi mume na mke wote wanachangia harusi.

Na wengine wengi tu hata harusi hawafanyi. Wanaona si lazima.
 
Kwanza, kugharimia harusi si mahari.

Pili, hata Marekani, hizo ni tamaduni zilizopitwa na wakati, siku hizi mume na mke wote wanachangia harusi.

Na wengine wengi tu hata harusi hawafanyi. Wanaona si lazima.
Ndio maana nikakuuliza mtazamo wako kuhusu mahari ni upi.

Kama unasema hiyo sio mahari, basi tuishie hapo.
 
Well
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…