sumbai
JF-Expert Member
- Jun 16, 2014
- 19,955
- 45,207
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Naona hujaelewa swali.
Hivyo hujaweza kulijibu.
Halafu unaishi katika ulimwengu wa kijima ambao mwanamke anamhudumia mwanamme.
Kama mahari ni shukrani kwa wazazi au walezi, mbona inatolewa kwa wazazi wa mwanamke tu?
Mbona hakuna kubadilishana mahari, mwanamme ashukuru wazazi wa mwanamke na mwanamke awashukuru wazazi wa mwanamme?
Kwani wazazi wa mwanamme hawastahili shukurani?
Kwann Kaka yangu Kiranga with due respect unapendaga kwenda opposite na tamaduni na dini??
Usiseme sijajibu swali Ila sijakwenda Sawa na mtazamo wako.
Mwanaume ndiye anayeoa anakuchukua MTU kutoka kwenye ukoo wake kuja kwenye ukoo wako. Mke anahama kwake anakuja kwako ndio maana wewe unalipa kamahari flani kushukuru Kwa malezi ya binti Yao.
Mkuu ulilipa mahari kiasi flani unapungukiwa nini??
Kama umempenda mwanamke utalipa tuu.
Ni ishara ya heshima.
Tujifunze kuheshimu Mila na destruri zetu.