- Thread starter
- #41
Kabisa mkuu, kazi ilikuwa na heshima sana, maafisa waliwanyenyekea raia na kuwathamini, maafisa wa TISS wa enzi zile walijua kujishusha na kuishi na watu vizuri
Zimekwenda zama zile ambapo rais alikuwa Nyerere, wasiojulikana hawakuzurura mitaani kupoteza watu, kina jenerali Sabaya hawakupata dhamana za uongozi, katiba ya nchi ilikuwa msahafu na kipaumbele, tukishindana na kushawishiana kwa hoja.