Wale mliokimbilia kujenga Dodoma poleni sana

Mkuu usidanganye bila uwepo wa Serikali hakuna kitu kumbuka mji umechangamka sababu ya Serikali Dodoma hakuna biashara yoyote ya maana labda utalii madini nk mji umekua sababu ya Serikali kuhamia huko
 
Hivi kuna watu walienda kuwekeza chato? Au unaongea jokes?
Kama ni kweli basi Bora walionda kujenga Dodoma kuliko hao
Usalama wengi walienda Chato kuwekeza nyumba kule analipwa posho analazimishwa anunue kiwanja kulekule kumuunga mkono Mheshimiwa. Usiponunua lazima akuzingue kule wametelekeza viwanja kuna wenyeji walikuwa wanakomaa kuuza viwanja anakataa 10M sasa hivi anabembeleza hata 1M akuachie kiwanja.
 
Aisee hatari sana
 
Kumbe mpumbavu mmoja anaweza kusababisha marumbano na wote mkaingia kwenye mtego wake.Thamani ya ardhi inaongezeka kila siku, pata muda ongea na wazee wakupe historia ya mji unaoishi sasa hutodharau thamani ya ardhi.Dar kilikuwa kijiji cha Washomvi leo ni jiji. Vivyo hivyo Dodoma,Singida,Igunga etc yatakuwa cities na wengi watakimbilia huko it's just matter of time YATATIMIA!!!
 
Sasa yeye si amezoea Bahari...Amezaliwa kwenye bahari, amekulia huko, akasoma hukohuko kwenye bahari...maisha yake mengi ameishi karibu na bahari....ndio maana anapenda maeneo yalio karibu na bahari...ni haki yake....
Maamuzi ya kitaifa hayaba mahusiano na mtu alipozaliwa au alipokulia ndio maana wafanya kazi wa serikali wanaweza kuzaliwa dar wakapangiwa ofisi kantalamba
 
Ila ukweli unabaki palepale kwamba wanawake wa kigogo wengi wao wana mawowo....kama unabisha ingia soko la sabasaba kule kwa wale akina mama wanaochuuza mboga za majani......
 
Watu waache kujenga wategemee kuishi kwenye nyumba za kupanga? Hapo Dar mbona Kodi za nyumba ziliporomoka ,mahoteli yakageuzwa hostel za madenti na bado mambo magumu?

Kesi ya uchumi ulioharibiwa na sera mbovu za mwendazake uliathiri Nchi nzima,hadi leo hii bado bei ya ardhi na nyumba iko chini na vyote havitoki kama zamani.

Na hata bank ukiweka collateral ya ardhi Unapata vihela kiduchu.Uchumi umeharibika ni mpaka ukiwa poa.Imagine saizi kuna Hali ya ukame hivi unategemea ardhi na nyumba zitakuwa na bei?
 
Miji inaibuka yenyewe au kuanzshwa kwa mikakati maalum ya kibiashara, ulinzi, au matakwa mengine muhimu ya kijamii.

Miongo kadhaa iliyopita,wafanya biashara wa Marekani walitengeneza mikakati madhubuti ya kuanzisha jiji la Las Vegas jangwani Sierra Nevada mahsusi kwa biashara za kamari, ukarimu na utalii.

Mikakati hiyo ilikuwa pamoja na kuhakikisha serikali ya jimbo inatunga na kupitisha sheria zinazoleta nafuu ya kodi inayotozwa kwa wadau wa biashara hizo hasa ile ya kamari ili kuvutia uwekezaji wa casino na waraibu wa kamari kwenye jiji hilo.

Sasa hivi, jiji la la Las Vegas ni moja ya majiji yenye usitawi mkubwa kabisa duniani!

Swali ni je, vipi Dodoma? Kulikuwa na mikakati ya ki kibashara, kiulinzi na usalama inayokidhi? Je kulikuwa na sera maalum za kuhakikisha mji unastawi na kukua, pia kuweka mazingira yanayoburudisha akili, roho na mwili(aesthetic)?
Kama zilikuwepo zilitekelezwa?
(Hapo natumaini wengi tunafahamu habari za CDA).

Nimalizie tu kwa kusema nimeona wengi wanaomsuta mleta uzi wakijigamba kuwa upangaji wa nyumba ni ghali na unatazamiwa kupanda zaidi. Niwaulize, huo ni mkakati wa kukuza mji huu mkuu ambao umedorora miaka yote hiyo mpaka rais wa awamu ya tano, mh. John Joseph Pombe Magufuli(R I P) alipofanya kile ambacho watangulizi wake(ukiacha baba wa taifa) walikupuuzia?

Mikakati ya kuufanya Dodoma uwe makao makuu ya nchi, achilia mbali kuwa tu mji wenye ustawi ina mapungufu mengi na serkali na wadau wengine inabidi wajipange upya.
 
Ok
 
Ok
 
Ok
 
Dah
 
Duh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…