Wale mliokimbilia kujenga Dodoma poleni sana

Wale mliokimbilia kujenga Dodoma poleni sana

Mimi dodoma nimeishi napajua vizuri
Ila ukweli ni kwamba dodoma ni kugumu na mzunguko wa hela ni mdogo
Hata Dsm ilishawahi kuwa na mzungumko mdogo wa pesa, shida yako unalinganisha mji wenye watu milioni 7 na wenye watu chini milioni moja.... haiiwezi kulingana. Lakini in a long run, utakuja kuwa na mzunguko mzuri wa fedha.
 
Dodoma ninavyoiona ni kama mji wa kutengenezwa,Dar ni mji uliojitengeneza wenyewe,miji iliyojitengeneza yenyewe kibiashara haitetereki .....mpaka hapo haiwezi kuja kuwa sawa kibiashara hata uko mbeleni
 
Mmhhh we ndio wale wale umezaliwa pwani,umesoma pwani,umeoa pwani mzaramo mwenzio,hujawahi kuvuka zaidi ya chalinze,Dodoma huijuhi.
Dodoma nyumba zinatafutwa kwa udi na uvumba,na soko,demand ya kupanga ni kubwa sana,
Mi mdau wa nyumba,kuanzia kisasa,area c,uzunguni,meliwa,mtumba,kote huku vyumba na nyumba zinatakiwa sana na mahitaji ni makubwa.
Usisikilize story za vijiweni.Tembelea Dodoma ujionee,fika eneo linaitwa kisasa ujionee,
Watu wanakuja wanaona nyumba,wanapanda dau wakupe 600K kwa mwezi,wachukue nyumba kwa miaka mitano,we amia kwingine!!
Mengine yamezaliwa mikoani mbali tu,yamefika Dar ukubwani yanajifanya kuiponda Dodoma ,utafikiri yamezaliwa Dar kumbe mikoa ya pembezoni huko
 
Miaka 10 ijayo Dodoma itakuwa imeshaipita Dar....uwekezaji unaofanyika kule ni Mkubwa. Uwezekaji wa Dar ni watu binafsi tu. Dodoma serikali inawekeza, na watu binafsi wanawekeza.
Kuipita Dsm sio kweli ila ndio litakuwa jiji labda linaloifuatia Dsm.
 
Umekuja mbio na mapovu kibao lakini hujaweka ushahidi wowote to back up your story..
We nawe [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji3][emoji6]!!!!
 
Miaka 10 ijayo Dodoma itakuwa imeshaipita Dar....uwekezaji unaofanyika kule ni Mkubwa. Uwezekaji wa Dar ni watu binafsi tu. Dodoma serikali inawekeza, na watu binafsi wanawekeza.
Hatutaiona Dodoma ikiiipita Dar katika miaka 100 ijayo
 
Ni upuuzi uliopitiliza kuwekeza mji mgumu kama Dodoma...nyumba hazina soko kabisa..wawekezaji aka shoppers plaza wanajuta manake manunuzi ni watumishi wa umma ambao matumizi yao ni ya msimu na wana nguvu ndogo...Bakharesa na Mo wameshindwa kuweka depot za maana Dodoma....maji hakuna,vumbi,mpauko...yule mwehu ametupa mateso sana
Hivyo vyote ulivyotaja vinarekebishika kabisa.... kwani ni afadhali kuongezewa nguvu kuliko kusingefanyika kitu... kuipeleka Serikali Dodoma ndio kuibadili Dodoma...
 
Hata Dsm ilishawahi kuwa na mzungumko mdogo wa pesa, shida yako unalinganisha mji wenye watu milioni 7 na wenye watu chini milioni moja.... haiiwezi kulingana. Lakini in a long run, utakuja kuwa na mzunguko mzuri wa fedha.
Sema patakuwa pazuri kuliko Shinyanga, Singida Songea lakini usiseme Dar.
Dar es Salaam ni future Mega City of the World
 
Mambo yanajiset taratibu. Ila kiukweli Dodoma ni Jangwa, mvua hazinyeshagi. Hao wala bata wa serikali walijiadhibu wenyewe kurudi huko.
Huko ambako mvua zinanyesha, mbona ukifika wakati wake mnazichukia????
 
Basically hali ya hewa kwa kipindi Fulani cha mwaka sio nzuri sana!! Pia ilikuwa hakuna umuhimu sana kwenye dunia ya Mtandao kuwarundika na kuweka wizara zote sehemu moja!! Kwa mawazo ya walio wengi ingependeza wizara ziwe kama ifuatavyo; Hazina DSM, uvuvi Mwanza, Utalii Arusha, Uchukuzi DSM, Misitu Morogoro, Madini Geita, Tamisemi mama LA mawizara Dodoma, Elimu Dodoma, Muungano na Mambo ya nje DSM
Wazo zur I'la huduma hata kwa online ipatikane si lazima kufika mkoa flani
 
Basically hali ya hewa kwa kipindi Fulani cha mwaka sio nzuri sana!! Pia ilikuwa hakuna umuhimu sana kwenye dunia ya Mtandao kuwarundika na kuweka wizara zote sehemu moja!! Kwa mawazo ya walio wengi ingependeza wizara ziwe kama ifuatavyo; Hazina DSM, uvuvi Mwanza, Utalii Arusha, Uchukuzi DSM, Misitu Morogoro, Madini Geita, Tamisemi mama LA mawizara Dodoma, Elimu Dodoma, Muungano na Mambo ya nje DSM
Huo utakuwa ujinga wa Hali juu sana,mutu ana shida wizara ya Afya ,mfano wako ,hiyo iwe morogoro,akifika hapo anaambiwa tunahitanji hiki kutoka wizara ya elimu,Sasa wizara hiyo iwe kagera-bukoba huko,huoni kama ni usumbufu wajinga sana huo,nilishawahi kuomba uhamisho kutoka Kwa katibu mkuu(wizara fulani-siitaji),nikaambiwa nenda Kwa katibu mkuu tamisemi,Sasa fikiria Mmoja awe mtwara na mwingine awe kigoma na wewe uwe umetokea mara usumbufu unaoupata ukoje?,vitu vingine mfikiri kabla ya kutoa comment,wizara ukizitawanya hivyo raia na maskini ndo wataumia,ukifika hapa unaambiwa nenda wizara fulani kwanza,Sasa hapo ziwe mbalimbali utakufa na shida yako
 
Mleta mada anawaza kwa urefu wa pua yake. Hizi mindset ni za kupuuzwa kabisa.
 
Mtoa post ipo siku atakuja kuandika....Serikali inaipendelea Dodoma, atakuwa analalamika sasa.
 
Back
Top Bottom