JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 7,808
- 16,972
Mmhhh we ndio wale wale umezaliwa pwani,umesoma pwani,umeoa pwani mzaramo mwenzio,hujawahi kuvuka zaidi ya chalinze,Dodoma huijuhi.Kipindi Serikali au mtu mmoja aliyeamua katangaza Dodoma kama makao makuu kwa maslai yake, watu wa Mikoani wakakurupuka kutoka huko kwenda kuwekeza Dodoma, sasa mambo yamekuwa magumu wanalalamika [emoji3] biashara zimekuwa ngumu na ni za msimu.
Nyumba walizojenga hazina wapangaji yaani mambo ni tafrani apeche alolo
Watu waliokimbilia huko wanalia wanapauka kwa vumbi na jua, Maji yamejaa chumvi hata kuyanywa ni shida
Ndo mkome kukurupuka kama chafya bila kufikiria.
Hizo nyumba zibebeni mzilete huku kigamboni [emoji4]
Unakimbia Dar unaenda kuwekeza Dodoma sehemu ngumu vile una akili kweli bora ungeenda kuwekeza Arusha, Mwanza, Moshi, Mbeya, Dar
Dodoma nyumba zinatafutwa kwa udi na uvumba,na soko,demand ya kupanga ni kubwa sana,
Mi mdau wa nyumba,kuanzia kisasa,area c,uzunguni,meliwa,mtumba,kote huku vyumba na nyumba zinatakiwa sana na mahitaji ni makubwa.
Usisikilize story za vijiweni.Tembelea Dodoma ujionee,fika eneo linaitwa kisasa ujionee,
Watu wanakuja wanaona nyumba,wanapanda dau wakupe 600K kwa mwezi,wachukue nyumba kwa miaka mitano,we amia kwingine!!