Wale mliokimbilia kujenga Dodoma poleni sana

Wale mliokimbilia kujenga Dodoma poleni sana

Mmhhh we ndio wale wale umezaliwa pwani,umesoma pwani,umeoa pwani mzaramo mwenzio,hujawahi kuvuka zaidi ya chalinze,Dodoma huijuhi.
Dodoma nyumba zinatafutwa kwa udi na uvumba,na soko,demand ya kupanga ni kubwa sana,
Mi mdau wa nyumba,kuanzia kisasa,area c,uzunguni,meliwa,mtumba,kote huku vyumba na nyumba zinatakiwa sana na mahitaji ni makubwa.
Usisikilize story za vijiweni.Tembelea Dodoma ujionee,fika eneo linaitwa kisasa ujionee,
Watu wanakuja wanaona nyumba,wanapanda dau wakupe 600K kwa mwezi,wachukue nyumba kwa miaka mitano,we amia kwingine!!
Mimi dodoma nimeishi napajua vizuri
Ila ukweli ni kwamba dodoma ni kugumu na mzunguko wa hela ni mdogo
 
Basically hali ya hewa kwa kipindi Fulani cha mwaka sio nzuri sana!! Pia ilikuwa hakuna umuhimu sana kwenye dunia ya Mtandao kuwarundika na kuweka wizara zote sehemu moja!! Kwa mawazo ya walio wengi ingependeza wizara ziwe kama ifuatavyo; Hazina DSM, uvuvi Mwanza, Utalii Arusha, Uchukuzi DSM, Misitu Morogoro, Madini Geita, Tamisemi mama LA mawizara Dodoma, Elimu Dodoma, Muungano na Mambo ya nje DSM
Exactly
 
Kipindi Serikali au mtu mmoja aliyeamua katangaza Dodoma kama makao makuu kwa maslai yake, watu wa Mikoani wakakurupuka kutoka huko kwenda kuwekeza Dodoma, sasa mambo yamekuwa magumu wanalalamika [emoji3] biashara zimekuwa ngumu na ni za msimu.

Nyumba walizojenga hazina wapangaji yaani mambo ni tafrani apeche alolo
Watu waliokimbilia huko wanalia wanapauka kwa vumbi na jua, Maji yamejaa chumvi hata kuyanywa ni shida
Ndo mkome kukurupuka kama chafya bila kufikiria.

Hizo nyumba zibebeni mzilete huku kigamboni [emoji4]

Unakimbia Dar unaenda kuwekeza Dodoma sehemu ngumu vile una akili kweli bora ungeenda kuwekeza Arusha, Mwanza, Moshi, Mbeya, Dar
Tatizo lako huoni mbali.... unaangalia na kunaona kwa urefu wa pua yako😂🤣😹
 
Dodoma ni mji mzuri sioni ubaya wake kihivyo. Pia kuhusu nyumba , Dodoma Kuna uhaba mkubwa wa nyumba na gharama za kupanga ni kubwa Sana.
Nyumba ya kawaida tu si chini ya 300k
Na hii haijatokana na serikali kuhamia huko bali ndio maisha ya huko yalivyo kwa muda mrefu.
Dodoma ni mji wa gharama Sana
Pia kuhusu Dar, watu wote hawawezi kuishi dar. Watu wapo wanafanya kazi namanyere, kalambo, tandahimba, buhigwe, ngara, uvinza n.k na maisha yanaenda vizuri tu.
Wote hao wakiwa na mawazo Kama yako basi hakutakua na Maendeleo.
 
Back
Top Bottom