Wale mliokimbilia kujenga Dodoma poleni sana

Mtu ambaye haoni fursa ya kuwekeza Dodoma naweza nikasema, ana macho ya kimasikini au hajawahi kutembelea miji mikubwa Duniani....

Dodoma in next 10 to 30 years itakuwa kama mji Mkuu wa Botswana...
Miaka 10 ijayo Dodoma itakuwa imeshaipita Dar....uwekezaji unaofanyika kule ni Mkubwa. Uwezekaji wa Dar ni watu binafsi tu. Dodoma serikali inawekeza, na watu binafsi wanawekeza.
 
Wabongo ni watu WA kukata Tamaa mapema Sana,mtoa mada ameshindwa kuona kesho itakuaje sidhani kama Dodoma kuendelea kwasababu baada ya miaka mitano ijayo huo mji utapiga hatua kubwa za kimaendeleo alafu sikuzote ardhi ni Mali na hata hao ambao wamejenga Huko Dodoma bado hawajapoteza pesa zao...
Maana ya uwekezaji ni kurisk maisha
 
Sasa kwanini dodoma isiwe makao makuu, hangaya anapenda tuu kukaa dar ila maamuzi ya kuhamia dodoma yalikuwa sahihi
Sasa yeye si amezoea Bahari...Amezaliwa kwenye bahari, amekulia huko, akasoma hukohuko kwenye bahari...maisha yake mengi ameishi karibu na bahari....ndio maana anapenda maeneo yalio karibu na bahari...ni haki yake....
 
Mtoa Uzi acha bias, Dodoma kuchele aisee fanya uende ukajionee mitaa you ipo full ...makulu sijui wapi na wapi
 
STRAGETICAL DOM HAPAFAI HAPAFAI HAPAFAI PALILAZIMISHWA TU NA HUU NDIO UKWELI HALISI LETS NATURE LEADS AND SHOW THE WAYS
 
Ni upuuzi uliopitiliza kuwekeza mji mgumu kama Dodoma...nyumba hazina soko kabisa..wawekezaji aka shoppers plaza wanajuta manake manunuzi ni watumishi wa umma ambao matumizi yao ni ya msimu na wana nguvu ndogo...Bakharesa na Mo wameshindwa kuweka depot za maana Dodoma....maji hakuna,vumbi,mpauko...yule mwehu ametupa mateso sana
 
Mkuu kwa nini kupangia watu maisha, kama wewe umejenga Dar wengine wanaona Dodoma panawafaa......
 
Mtu ambaye haoni fursa ya kuwekeza Dodoma naweza nikasema, ana macho ya kimasikini au hajawahi kutembelea miji mikubwa Duniani....

Dodoma in next 10 to 30 years itakuwa kama mji Mkuu wa Botswana...
Hakuna kitu kama hicho...Dom haiwezi julian kiuchumi sababu hakuna vichocheo vyovyote....ukiona mji hakuna wachina wala wazungu ujue ni pakishenzi
 
Hii nakataa nina shughuli nafanya dom, mzunguko wa pesa popote pale hutegemea unachofanya. Hata dar unapoona Kuna mzunguko mkubwa, Kuna watu wanafeli na kufunga biashara.
Labda kama una deal na wanafunzi na watumishi ...ndiyo utatoboa Dodma
 
Miaka 10 ijayo Dodoma itakuwa imeshaipita Dar....uwekezaji unaofanyika kule ni Mkubwa. Uwezekaji wa Dar ni watu binafsi tu. Dodoma serikali inawekeza, na watu binafsi wanawekeza.
Uwekezaji wa miundo mbinu?wakati hakuna cha bandari,viwanda,utalii,etc?
 
Dodoma hakuna vichocheo vya kiuchumi..maendeleo yatatoka wapi?
 
wewe una matatizo yako,tena yanachangiwa na umasikini.ulipoanza tu kusema mtu alitangaza kuhamia dodoma kwa maslahi yake,tayari nikashtuka kwamba jitu lililoleta mada ni tofali kiasi gani.

dodoma bado ni makao makuu,na ujenzi wa nyumba haujawahi kuwa hasara palipo na watu,wewe endelea kuwekeza qnet ndiko wajanja wamejaa huko wanapakua pesa kwa laptops na smartphones.
 
Mimi nilikuwa Dodoma hivi karibuni, aisee panachipuka kwa kasi ya ajabu.........ni swala la serikali kuweka jitihada zaidi za kuweka miundombinu muhimu kwa ajili ya hadhi ya makao makuu, nilichogundua pia hali yake ya hewa imeboreka sana tofauti na zamani, na majuzi hapa makamu wa rais alikuwa anahimiza uzalishaji wa vitalu vya miti ili taasisi za umma na binafsi, wafanyabiashara na wananchi wapande miti ya kutosha........kwa hiyo ndugu mleta mada unapo underrate Dodoma unakuwa hueleweki hasa lengo lako ni lipi, labda kama una chuki binafsi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…