Wale mliokimbilia kujenga Dodoma poleni sana

Tatizo mmeingia dar juzi ndo mnapiga kelele. Hivyo viwanja unavyonunua kwa square meter kibada wenzio tulinunua kama mashamba tena kwa kubembelezwa miaka ya 2003. Tembeni muelimike. Nyie kaeni na dar yenu mtakuja shtuka wenzenu washakuwa mabilionea
Nani kazungumzia kibada hapa? na ujanja wako wa kununua mashamba 2003 umeyafanyia chochote cha maana? hayo mashamba kalime Nala na Mtumba huko jangwani, tuliza mihemko
 
Watu wamejenga wenyewe then unasema mwendazake ndo kaboresha acha ujinga wewe n jitihada za watu binafsi wala sio yeye
wewe ndio una akiri, tuambie una nyumba ngapi?

Acha ujinga mbuzi wewe
 
Nani kazungumzia kibada hapa? na ujanja wako wa kununua mashamba 2003 umeyafanyia chochote cha maana? hayo mashamba kalime Nala na Mtumba huko jangwani, tuliza mihemko
Ndo maana nimekuambia wewe ni wa kuja lazima tukupanguse ushamba. Hiyo dar unayoiona ya maana na viwanja unavyonunua kwa mita sisi tushanunua kitambo kama mashamba.
Kwa habari yako huko kigamboni kote ilikuwa nimashamba tu . Ujanja sio kusifia mji. Hata hiyo dar unayojitapia watu tushawekeza kitambo kipindi wewe bado ni form nyoya
 
Nani kazungumzia kibada hapa? na ujanja wako wa kununua mashamba 2003 umeyafanyia chochote cha maana? hayo mashamba kalime Nala na Mtumba huko jangwani, tuliza mihemko
Haha kama umeota nikuuzie viwanja vingapi na vipi na dar unataka kiwanja nikuuzie
 
1.Foleni kubwa bank sio utibitisho wa kuwa na wateja wengi. Bank nyng hapa Tz hasa hizi traditionalbanks zina huduma mbovu na za kimazoea. Usishangae kwenda bank unakuta foleni ndeefu ya watu kumbe wote wamefata bank statement na wameambiwa mtandao unasumbua kwa hyo wasubiirie na wanaweza kaa hata masaa mawili. (Huwa na najiuliza department ya IT kwny hz bank inafanya kaz gan?

*Hvyo unaweza kuta watu wako bank kwa sabab wanasubr huduma flan over a time kwa hyo wanarundikana na kuonekana wengi lakn kama wangehudumiwa na kuondoka huwez kuta hata watu wa5 kwny foleni

2.Basi za luxury dodoma ni Shabiby, ABC na kimbinyiko only. Hyo happy nation unayozungumzia ur utterly wrong.
Bm Coach siyo lakishari?
 
Hii mada inaonesha kumbe watu wengi bado wana mtazamo hasi dhidi ya mji wa Dodoma.

Binafsi mara ya kwanza nimefika Dodoma miaka 26 iliyopita. Kweli wakati huo maisha yalikuwa magumu sana kuishi Dodoma kwa sababu zifuatazo;
Mosi, mji ulikuwa ni mfinyu mno, ulikuwa unaweza kutumia dk zisizozidi 40 ukatembea mji mzima.
Kipindi hicho hata daladala hazikuwepo.

Pili, maji yalikuwa ya shida sana kiasi kwamba tulilazimika kufukua makorongoni kutafuta maji. Hali hiyo ilichangia sana kuwepo kwa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa macho, kipindupindu, homa ya matumbo n.k.

Tatu, sehemu kubwa ya mji ulikuwa ni jangwa hali iliyopelekea kuwa na hali mbaya ya hewa hasa kipindi cha kuanzia mwezi Mei hadi Julai.

Nne, mzunguko wa fedha ulikuwa mdogo kutokana na kukosekana kwa shughuli za uzalishaji mali.

Kuanzia mwaka 2018 hali imekuwa tofauti. Changamoto nilizozibainisha hapo juu sasa zimefanyiwa kazi. Mji umekuwa sana na miundombinu ya kisasa imewekwa.

Dodoma kwa sasa hakuna nyumba iliyokamilika yenye kuhitaji wapangapi ikakosa wapangaji tena kwa bei nzuri ukilinganisha na bei katika miji mingine ya nchi yetu.

Hata suala la usafiri sasa hivi limeboreshwa sana. Kwa upande wa usafiri wa anga, zamani ili kupanda ndege mfano kwenda Dar au kokote ilikubidi ukodi ndege nzima ambapo nakumbuka mwaka 2011 tulikuwa na na shida ya haraka kwenda Arusha ili ilibidi tukodi ndege nzima kwa Tshs 6,000,000/ kutoka shirika la ndege la MAF. Sasa hivi Dodoma kupitia mashirika ya ATCL na PRECISION karibu kila siku kuna safari za kwenda miji yote muhimu kutokea Dodoma tena kwa bei nafuu.

Dada hivi kupitia mpango kabambe wa kuendeleza mji wa Dodoma inatarajiwa kuanzishwa usafiri wa treni za mjini (commuter) utakaounganisha maeneo yote muhimu kuanzia Ikulu, mji wa kiserikali, uwanja wa ndege Msalata, stendi ya mkoa na mjini kati.

Pia sasa hivi serikali inaendelea na ujenzi wa majengo 24 ya ghorofa 6 ya wizara mbalimbali katika mji wa kiserikali Mtumba sambamba na ujenzi wa barabara za lami katika mji huo na maeneo mengine.

Jambo pekee linalohitaji kufanyiwa kazi na mamlaka za jiji na wakazi ni kuhakikisha tunaongeza kasi ya upandaji miti na kuitunza iliyopo kwani kupitia miti hiyo sasa hivi hali ya hewa na mandhari ya mji ni ya kuvutia tofauti na zamani. Pia mradi wa kuchukua maji ziwa Victoria na kuyaleta Dodoma ukitekelezwa kama serikali ilivyoahidi mji utakuwa wenye kuvutia zaidi kwani maji ya ziwa Victoria ni baridi kupita haya tunayoyatumia sasa.

Fursa za uwekezaji katika mji huu ni nyingi kuanzia nyumba za makazi, shule za binafsi, viwanda vya kukamua/ kusindika/ kukoboa mazao kama zabibu, alizeti, mahindi, mchele, ubuyu n.k. Pia kutokana na uwepo wa vyuo vingi kuku na mayai vinahitajika sana.

Dodoma sio pa kusimuliwa, fika mwenyewe ujionee na uwekeze kabla hujachelewa kwani miaka mitano ijayo hata Gaborone Botswana itakuwa imepitwa.
 
Duh,umejibu Kama msemaji wa jiji la Dodoma..vyema
 
Usisahau kuna waliowekeza Mtwara enzi za gesi, betting ilianza kitambo sana
 
Tatizo lako umekariri maisha nyumba unaweza kujenga hata kijijini inategemea malengo yako kuna watu wanaangalia miaka 10 au 20 ijayo na kuendelea wewe akili yako imelala na umekalili kuwa miji mikubwa ndipo unatakiwa kujenga, nikupe pole ila ujue Dodoma kuna uhaba mkubwa wa nyumba na hata serikali haitahama Dodoma, Rais Samia ameshatoa pesa kwa kila wizara ijenge ofisi ya kudumu Dodoma
Kuchukua viwanja na kujenga ni uwekezaji wa mda mrefu na mzuri,zamani Tabata ilikuwa pori ,kuna watu walijenga na kuchukua viwanja vikubwa sasa hivi wanakula faida,watu wanachukua viwanja nje ya mji tena viwanja vikubwa ,baada ya miaka miwili anakupimia 20*20 Bei ghali .
 
Back
Top Bottom