wastani kwa idadi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 503
- 1,432
1. Simu - Ni biashara iliyoshamiri sana kwenye vitu used lakini wengi zimewingiza kwenye matatizo, mtu kanunua simu laki 4 au zaidi haoni shida kutoa elf 50 polisi waifatilie, yani ukinunua simu iliyoibiwa ukipachika tu laini yako tayari ushadakwa kwa taarifa zako ulizosajilia laini na makadirio ya sehemu ulipo kwa mnara unaotumia, pia ni kawaida yetu watanzania kumtia adabu mwizi hivyo tegemea alieibiwa kukubambikia kesi ya ziada kwamba ulimuibia pesa ambazo inabidi umrudishie, wengine wanaishia mahabusu ama jela kwa miaka.
2. TV - Hasa hizi za bei ghali kuanzia milioni, Sikuhizi zinafungwa gps, ukiwasha tu nayo gps inaanza kusoma sehemu ulipo, mlangoni utasikia hodi ukifungua mlango tegemea ugeni wa maafisa wa usalama, Hapa moja kwa moja wewe ni mtuhumiwa wa wizi,
3. Pikipiki - Nazo zinafungwa gps, ile michezo ya zamani ya kuiba Mkoa X kuuza Mkoa Y imepitwa na wakati ikiwa mtu kafunga gps, watakufungia safari mpaka sehemu ulipo