Wale mnaopenda kununua vitu used muwe makini sana, epuukeni zaidi kununua hizi bidhaa zinaweza kuwatia ndani ama kutoboka mifuko.

wastani kwa idadi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
503
Reaction score
1,432
1. Simu - Ni biashara iliyoshamiri sana kwenye vitu used lakini wengi zimewingiza kwenye matatizo, mtu kanunua simu laki 4 au zaidi haoni shida kutoa elf 50 polisi waifatilie, yani ukinunua simu iliyoibiwa ukipachika tu laini yako tayari ushadakwa kwa taarifa zako ulizosajilia laini na makadirio ya sehemu ulipo kwa mnara unaotumia, pia ni kawaida yetu watanzania kumtia adabu mwizi hivyo tegemea alieibiwa kukubambikia kesi ya ziada kwamba ulimuibia pesa ambazo inabidi umrudishie, wengine wanaishia mahabusu ama jela kwa miaka.

2. TV - Hasa hizi za bei ghali kuanzia milioni, Sikuhizi zinafungwa gps, ukiwasha tu nayo gps inaanza kusoma sehemu ulipo, mlangoni utasikia hodi ukifungua mlango tegemea ugeni wa maafisa wa usalama, Hapa moja kwa moja wewe ni mtuhumiwa wa wizi,

3. Pikipiki - Nazo zinafungwa gps, ile michezo ya zamani ya kuiba Mkoa X kuuza Mkoa Y imepitwa na wakati ikiwa mtu kafunga gps, watakufungia safari mpaka sehemu ulipo
 
Simu najua..gari la show room linaweza kuwa la wizi?

Yaan nanua la wizi limefungwa GPS ma mm nafunga yakwangu ninini kitatokea. Ya kwake inasoma na huku yangu inasoma
 
Simu najua..gari la show room linaweza kuwa la wizi?

Yaan nanua la wizi limefungwa GPS ma mm nafunga yakwangu ninini kitatokea. Ya kwake inasoma na huku yangu inasoma
Ukinunua gari show room la wizi lenye gps, ukiweka na yako, kila moja ataiona yake, ikiwa alieibiwa akakukamata kwa wizi wa gari hakikisha una nyaraka zote za kuonyesha umelinunua kwenye show room na TRA wanatambua hivyo, mwenye show room ndie itabidi ule nae sahani moja maana ni mtuhumiwa wa wizi.

Nyaraka, mkataba, risiti, n.k. zinazotambulika na serikali ndivyo vitakulinda.
 
Bado hamjajuwa tu....wenzenu hayo mambo tulishaachana nayo
Miaka 20 iliyopita

Ova
 
Gari za Show room Zina shida Kuna dada alinunua baada ya muda kadhaa Kuna jamaa wakamfuata kuwa tumekuja kutoa kakifaa ketu kwenye hili gari,Kumbe wenye show room walikuwa wamelichukulia mkopo somewhere
Simu najua..gari la show room linaweza kuwa la wizi?

Yaan nanua la wizi limefungwa GPS ma mm nafunga yakwangu ninini kitatokea. Ya kwake inasoma na huku yangu inasoma
ri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…