Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Basi oa mama wa nyumbani awe house maid wako.
Mbona ukimpata mwenye kaulewa kidogo ndoa inakuwa salama na amani na upendo tele kuliko hawa wanaojiita wasomi kushindana kwenye nyumba kila siku,

Yaani vikao vya wanaume kutokuwaoa tu, piga mimba mkalee huko tutaoa baki tatu
 

Upo sahihi kabisa kuna muda wa kufanya kwa nguvu zote kumsaidia mwenzako kwa kipindi cha majukumu mazito kama hayo!!

Ukweli ni kwamba ni vyema mke kukupelekea maji bafuni kuoga, kukupikia chakula kitamu upendacho, kukufulia n.k n.k, vyote hivi ni kwa ajili tu ya kunogesha penzi lenu!!

Ila kama haoni umuhimu wa mbwembwe zote hizo pia, siyo hasira na kuachana kabisa,,!!

Sioni shida kupeleka maji bafuni kuoga, kwanza siku hizi zipo shower unaenda unajimwagia tu chap,

Akishindwa kufua unafua tu mwenyewe siyo issue, inaweza kupunguza upendo wenu lakini siyo kesi!!!

Hajaweza kupika chakula upendacho, ukiweza jitengezee tu chap, au migahawa mingi wanatengeneza pita kula vzr rudi nyumbani, maisha yanaendelea,

Unaepusha mengi, akiweza kujiongeza sawa, akishindwa shauri yake!!
 
Uwiii kuku anapikwa na kinyeo duu pole ulitaka mama wa nyumbani sasa ukapata kilaza, [emoji41] angalia na watoto watakuwa hivyo hivyo tu.
 
Kivipi mkuu, Mimi mwanaume anayetaka eti kubebewa ndoo bafuni sijui kupika daily na nimetoka kazini kwangu naona hafai kuwa mume, zama zimechange sikuhizi wooi
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hujajua dhana ya kuishi wewe, unawaza kirahisi mno kuliko uhalisia wa mambo yenyewe.
Halafu sio kila mwanaume anayepiga kelele anaogopwa na kuheshimiwa. Kwa taarifa yako mke wangu hathubutu hata kufanya hivyo kwakuwa anajua
We sasa unataka familia zote za ukanda wa pwani wasiolewe
 
Mbona ukimpata mwenye kaulewa kidogo ndoa inakuwa salama na amani na upendo tele kuliko hawa wanaojiita wasomi kushindana kwenye nyumba kila siku,

Yaani vikao vya wanaume kutokuwaoa tu, piga mimba mkalee huko tutaoa baki tatu
Sawa.
Piga tu mimba kwani mtoto atakaezaliwa ni wa kuku huyo!
 
[emoji28][emoji28]..hii comment nimecheka sn asee

Watu mnapitia magumu sn .Mkuu pole sn

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Asantee sana Mkuu ..Sasa katuma ile pesa nmerudi safari kila siku malizia basi nipate iphone nikaona huyu manzi hanijui nimempiga kalenda na hela ninayo ya kutosha mpaka now ameanza kuniambia ohh kama vipi tuachane ..nikamuambia kwakuwa simu ni muhimu kuliko mimi pita hivi now nina wiki nalala kwa mchepuko wangu hajaniona analia tu kwenye sms ..hawa viumbe ni waajabu sana asee mkuu
 
Katika mahusiano yangu yote nimekuwa nikiwakwepa sana wanawake wenye kelele zisizo na mbele wala nyuma (No offense) Sikatai mwanamke akiwa anaongea sana, Je anaongea nini hilo ndio linalo matter.

Mfano mdogo kipindi cha mwaka 2006 Nilikuwa na mahusiano na binti flani wa kirwanda kwa kiufupi hayakuwa mapenzi kama mapenzi mwanzoni, lakini mimi ni mtu ambaye hata kama tukianzisha mahusiano kimasihara huwa kama kuna kitu nimekiona kwako huwa nageuza yawe serious.

So nilifanya hivyo, Yule mwanamke alikuwa na mapungufu mengi tu, japokuwa alinipenda, lakini yote niliyamudu isipokuwa mambo yafuatayo, Uongo uliokithiri, Ugomvi na Mdomo kama chiriku yaani sio muongeaji ni kidomodomo, anachukia anapojisikia tu na kukujibu ovyo.

Kwa mtu asiyejua angesema we jamaa umridhishi huyu mwanamke, Lakini nikuhakikishie Alikuwa anapandisha mlima wenye urefu wa meters 8,000 from above sea level na kufika juu mwisho wa urefu wa mlima mara 3 mpaka 6 bila Safari kukatishwa, kwahiyo hiyo haikuwa sababu kabisa.

Sasa Nakumbuka hiyo siku nilikuwa nimetoka kuoga nikakuta missed call 37 na sms 10 Zenye urefu kama huu uzi hapa.
Unajua zilikuwa zinasemaje?

Wewe mwanaume malaya sana, Utakuwa uko na wanawake zako, Najua mimi najua, Huwezi kukaa bila kut....na, hupokei simu zangu tayari uko kifuani kama hunipendi nambie. Siwezi kuandika zote lakini zilikuwa shutma nyingi sana.

Anaweza kudanganya hata kama ukweli hauna hasara, Unaweza kumuona mahali yuko anafanya jambo la kawaida tu, lakini ukamuliza uko wapi au unafanya nini Utajuta kwa jibu utakalopata. Nilimuona siku moja Samakisamaki Postal Anakula na yuko peke ake akanambia yupo kazini na kazi ni nyingi. Sio mara moja Vitu anavyodanganya ni vingi.

Nilizaa nae lakini Najuta na natamani nirudi nyuma nisawazishe nilipokosea, Ingawa tuliachana lakini kitendo cha kuacha alama pale huwa kinanipa mawazo sana.
 
Nilizaa nae lakini Najuta na natamani nirudi nyuma nisawazishe nilipokosea, Ingawa tuliachana lakini kitendo cha kuacha alama pale huwa kinanipa mawazo sana.

ukizaa na mwanamke/mwanaume ambaye mliokotana huko mabarabarani, inakuwa ni kama umetengeneza agano la kiroho na yeye.

hata kama ulikuwa humpendi, you will always be haunted by her/him whenever you go. mtoto wenu anakuwa kiungo cha kuwavuta pamoja.

kwa hiyo kuna siku mtajikuta mpo eneo moja ili kusolve jambo muhimu linalomuhusu mtoto.

inaweza kuwa kwenye ofisi ya mwalimu mkuu wa shule anayosoma, chumba cha hospital ambayo kalazwa, chumba cha mahakama, kituo cha polisi, ofisi ya ustawi nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…