Wale tuliokulia kwenye familia za kishua tukutane hapa

Mimi nimekulia ukapukuni kweli kweli, ila ilitokea katika maisha yangu situation mbili nilizojikuta nimefika kwenye mji wa washua.
1. Huyu kulikuwa na undugu kwa kiasi fulani, nilipofika kwake alikuwa mstaaf.

Nilikuwa napata habar zake kwamba kuna maisha duniani na anakula maisha mazuri mno! Siku nimefika kwake nikiwa mdogo mika ya 90+ la kwanza nililojifunza kumbe hakuna kumeza mboga, swala la kumeza mboga au kula mboga nyingi kuliko ugali ni agenda ya kimasikini tu, kwa matajiri unatakiwa ule tani yako ushibe.

Nimefika pale chakula kilivyotengwa likaletwa sufuria saafi mezani limejaa nyama ni tani yako kujipakulia kula utakavyo!

Toka siku ile pale nikajifunza kumbe ukiambiwa unameza mboga ni umasikini wetu tu.

Bahati mbaya sasa sijui kulitokea nini hii famili ilikuja kufilisika had ziro, yule mzee alipoumwa hata hela ya matibabu ilikosa akafa.


2. Huyu wa pili ilitokea tu mazingira nikajikuta nimefika kwake kwa situation fulani tu, yafuatayo niliyaona

(a) Pale nilimkuta kijana tunalingana na tulikuwa wote tumehitim form 4 mwaka mmoja ila yeye kala ziro yake safi na hana wasi wasi,
(b) Huyu dogo alikuwa ni kupiga honi house boy anafungua geti, akipark gari hili anaondoka na lingine

(C) Dogo chumban kwake akifungulia muziki nyumba inatetema, nilitaman nione ukubwa wa ule muziki ila ndo hivyo no connection

(d) ile familia house boy alikuwa kawekewa tv yake jikoni huko huko, enzi za ungo na tv za chogo, hatakiwi kuja seblen kuangalia tv kubwa, na chakula chake ni huko huko jikoni...
Sijufanikiwa nae kuongea nae sababu nilikaa siku chache na ndo hivo anashinda bustanini huko na kufungua mageti tu ilihal mm nashinda chumban nikitoka ni seblen nikisikia ukiwa narudi chumbani

(e) nnachokumbuka mzee alisema anahangaika dogo achague anachotaka akasomee nje huko na yupo katika harakat za kumbembeleza na kumukonvince..


(f) siku naondoka nilipewa elf 35,000


Haya wa kishua Mungu awabariki, lakin msidharau wasio navyo maana vyote hupatikana hapa hapa duniani na huachwa hapa hapa duniani..

JPM aliuza vile visamaki vidogo kichwani ila alikuja fika level ya Urais wa nchi..
 
Kwamba hakunaga kitu KUMEZA MBOGA ni umasikini tu
 
Kwamba hakunaga kitu KUMEZA MBOGA ni umasikini tu
Ndio Mkuu, maisha bora unalazimishwa kula, ukila finyango moja wanashangilia wororooooo leo kala sana kijana wetu,

Ww kijini tulipokulia finyango moja ukirudia ya pili unakatwa jicho kwamba unameza mboga, Ni UMASIKINI, MBOGA HAIMEZWI UNATAKIWA ULE UTOSHEKE IBAKIE YENYEWE
 
[emoji23][emoji23][emoji23]nipitie huku
 
Pia Kuna binadamu wabaguzi yaan unaenda Kwao wanakubagua mpk unajijua😂😂
Vyombo utakavyo pewa chakula vinaenda kutupwa.......

Nilicho jifunza Kuna watu wana be motivated by negative motivation........
 
Sisi kuna kipindi maisha yali yumba morng tulikuwa tuna kunywa chai na ndizi bokoboko kama unazijua tulikuwa tuna kula uku tunachekana [emoji23][emoji23] siku tukioona usiku ndizi kila mtu ana wai kulala
Ungekulia kwetu singida usingekula mwaka mzima mkuu. Nimekua nikiona ndizi ni chakula kizuri sana hata kipikweje 😅

Kule kwetu ni mwendo wa ugali mlenda, ugali na mboga za majani makavu weeee!
 
Mbna Kam ww dada angu kbsa mmesema kwenu wanaume watano mbn kam wee ssiter kbsa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
sijui familia ya kishua ni aina gani. mimi namshukuru Mungu nimefanikiwa kimaisha na vyote hivyo watoto wangu wanaenjoy, ila huwa siwalei kishua kabisa kabisa, kwasababu wale niliozaliwa nikijua wanaishi maisha ya kishua, ndio mawatu mapumbavu ya kutupa huku ukubwana, hayajui maisha kabisa kabisa, ni kama mandondocha tu. kuna mmoja nilisoma naye, babake alikuwa meja jenerari wa jeshi, he had everything. wakati tunasoma alikuwa ananikejeli mimi kwamba nikazane kwasababu babangu hana hata nyumba, mimi nilikzazana kwelikweli. nimekuja kukutana huku ukubwani, kumbe huyo dingi yake alishaga dead, mali waligawana, zilishasambaratika na ukimuweka pamoja na mimi wote tutafute maisha, nimemzidi mbali sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…