Wale tunaopenda vacation, sehemu gani ya utalii Tanzania uliyofika au unatamani kufika?

Wale tunaopenda vacation, sehemu gani ya utalii Tanzania uliyofika au unatamani kufika?

Ila wadau tuwe tunatembelea hata restaurants wikiend kwa kuwa ndio siku za free tusisahau kuenjoy ilihali tunahangaika kutafuta pesa.
 
Wale walikuwa wanauliza Dubai hii apa ya Dubai expo sijafwatilia vyema ukiweza cheki uone kama utaweza kwenda kuenjoy Dubai View attachment 1984992
Screenshot_20211024-090448.jpg
 
Wakuu vipi.
Msimu wa Christmas ndio huu,wapi pa kwenda kuenjoy weka comment yako ya mahali popote unapo pajua

Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app
 
Nimekupa Like Mkuu...
Ila Vacation wapi
Lushoto nasikia Kuna Hali ya Hewa Nzuri Baridi na Miti au kuna kingine?

Bagamoyo nasomaga tuu Kwenye history kuwa kuna Magofu na Nyumba za Kale, Sijui Kama Kuna Kingine! Au kuna Kingine?
Bagamoyo ni kama Tegeta tu, sema kuna wazungu, Ukishangaa utaishia kuona Vibanda vya tigopesa na MPESA.
 
ALL NATIONAL PARKS
Ni utaratibu niliouzoea toka kwa wazazi nampaka sasa nauendelezea Xmass kwenda sehemu tulivu kipindi cha sikukuu. My next vacation nitaenda Ruaha National Park coz zingine zote nchini nimeshafika nakufurahia utalii wa ndani. Mwaka mpya ni siku yakuonana ndugu wote kula, kunywa kwa pamoja na kubadirishana mawazo
 
Kwa hyo tuseme njia ya Lindi hadi mtwara hakuna maeneo ya Vacation? embu tupeni mchongo watu wa upande huo pia.
 
$1,000 si ni kwenye Tsh 2.3M kwahiyo kumbe inatosha kabisa kwenda na kuridi? Ngoja niache uzembe niingie hata Dubai kuhusu kulala nitalala hata stendi.

Sema nikirudi ntakuwa nimechoka sana hata hela ya daladala nitakua sina
hifadhi hata buku mbili ya kukodi boda toka pale airport hadi buguruni chama....la msingi utoke pale airport na boda...ukifika chama akili yako ita click ni vipi ufike kwenu.

ila hutakiwi kusafiri na begi kubwa, tembea na backpack huku ndani yake ukiwa umehifadhi jinsi zako mbili, t-shirt tatu na boxer nne, kibaharia flani hivi.
giphy.gif
 
Kama hujawahi kutoka nje ya nchi na unataka kuona dunia ya kwanza ikoje nenda Dubai. Gharama hazitishi na visa yake inapatikana kirahisi. Nauli kwenda na kurudi around $500, hotel siku 3/4 around $200, maana yake ukiwa na $1,000 unapata na pocket money $300.
Hiyo trip ya Dubai nimeipangia mwaka ujao mwisho wa mwaka. Mwaka Huu, kuanzia 25 Desemba naanzia na Bujumbura, niivinjari Burundi, nipande kaskazini kupitia Lake Kivu hadi Goma DRC. ... Safari ya kurudi nitapitia Kigali Rwanda...

Madereva wa magari ya mizigo "Transit" kutoka Tanzania waliomo humu JF, tuwasiliane ili niunganishe nao safari ya kurudi Dar es salaam... Nitaleta mrejesho.
 
Back
Top Bottom