Wale tunaopenda vacation, sehemu gani ya utalii Tanzania uliyofika au unatamani kufika?

Wale tunaopenda vacation, sehemu gani ya utalii Tanzania uliyofika au unatamani kufika?

2006; Mwanza/L. Victoria.
-Hotelini niliagiza chips yai, muhudumu akacheka, akaniambia hakuna chips yai bali kuna samaki, nikaagiza hiyo wakaniletea. Vichips vya kuhesabika ila bonge moja ya samaki, na ndo siku pekee niliyoshindwa kumaliza samaki.
-Hopefully nitarudi tena mwanza kutalii vizuri ziwa victoria.

2009; Zanzibar.
nilibahatika kutembelea;
*Stone town

*National museum of zanzibar
-Hapa nilipata historia ya utawala wa kisultani ya Zanzibar mpaka mapinduzi yalipofanyika
-nilibahatika kupanda mpaka gorofa ya kwanza kuangalia mfanano wa vyumba vya masultani na familia zao
-Gorofa ya tatu tuliambiwa imefungwa kwa sababu ilikuwa "unstable"

*Slave market

*Nyumbani kwa Sultani Barghash bin Sayyid Said
-huyu mwamba alikuwa na mke mmoja na hawara 99, alijenga swimming pools 3, kila moja wanakaa mahawara 33, wakiogelea uchi, wakati huo jamaa yupo chumbani kwake, gorofa ya pili akiwaangalia kupitia dirishani, akimwona amtakaye kwa muda huo anawaambia wafanyakazi wake wanamfuata na kumpeleka room kwa jamaa.
-Alikuwa akitumia aina fulani ya "alkasusu", ambayo tourguide alipata kutaja mchanganyiko wake pale (wadada walikuwa busy kuandika).

*Christ Church
-Hapa nilipata historia ya kuuma kidogo na kusikitisha ya watumwa
-Tukaoneshwa msalaba uliotengenezwa kutoka katika tawi la mti, ambao ulipandwa/kuota katika kaburi la David Livingstone kutoka huko zambia

*Prison Island
-watumwa walifikishwa hapa kabla ya kupelekwa kuuzwa pale slave market. Kwa wagonjwa ndo ilikuwa mwisho wa safari yao maana waliuliwa na kutupwa katika shimo kubwa lililo katikati ya kambi, likizungukwa na vyumba/jela za hao watumwa
-wale watumwa wababe hapo ndo palikuwa mahala pa "kuvunja(kuwa broken spiritually), kukatishwa tamaa, kuonesha kuwa njia pekee ya kuishi ni wao kuwa watumwa"
-kuna wanyama pia kama kobe, na jamii ya digidigi(sina uhakika). pia tulionesha kobe mmoja aliekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 90 mpaka 150.
-Ufukwe wa Prison island ulikuwa murua sana

Baya pekee katika safari/utalii wa zanzibar, tulienda muda/kipindi cha mfungo. Kwa hiyo swala la chakula hasa hasa kipindi cha mchana ilikuwa issue nzito.
 
2015;
Kinukamori waterfalls
-kiingilio nafuu(haikuidi 15,000/=)
-Mandhari nzuri, maji safi na ya baridi
-Historia nzuri pia
-Kulikuwa na wakenya wengi kuliko wazawa/watanzania wenzangu.

2016; Udzungwa Mountain Waterfalls
-Highest waterfalls in Tanzania.
-Kuna "Hiking trail" nzuri sana.
-Kuna aina nyingi za miti katika njia ya kupanda kufikia kilele cha waterfall hiyo, baadhi ni sumu na inaweza kukuua, njiani kuna vibao vya kuitambulisha miti hiyo, pia hiking guide anatoa maelezo.
-Ukifika kileleni, hali ya hewa ni safi sana yenye kaubaridi, tofauti na mlipoanzia chini. Pia unaweza ona mashamba (plantations) ya miwa.

Dec 2018 - Jan 2019; Dareda, Babati
Huu ulikuwa utalii wa Bahati(tuseme Accidental Tourism)
-Tulifika Dareda Mission hospital kwa ajili ya mafunzo ya mwezi mmoja, kuna guest room za hospital(15k), bafu maji ya moto, maana hali ya hewa kule ni ya ubaridi. kuna guest za nje ya hapo, bei ni 3000 mpaka 5000, ila sio za kuridhisha sana.
-Watu wa huko wanaladhufi fulani nzuri, pia maeneo yao huko yana majina kama sio ya kibongo eg Bashinet, Kwatabradik etc
-Kuna waterfalls nzuri tu, pia watu wanafanya kilimo cha umwagiliaji, chakula bei rahisi(kwa wapenzi wa nyama choma, hasa hasa ya mbuzi, huko ni murua sana).

Wapi Napenda kufika kwa ajili ya utalii
1. The African Great Lakes
*L. Victoria, L. Tanganyika. L. Nyasa
-Maziwa yetu haya yanashikilia rekodi kadhaa za kimataifa, jumuisha na mandhari pamoja na aina ya samaki wapatikanao humo(hasa L. Nyasa).
-Je, wajua kwamba umbali wa upana wa ziwa Nyasa kutoka fukwe za Tanzania) mpaka fukwe za Malawi, katika sehemu pana zaidi, ni sawa na umbali wa kutoka dar es salaam mpaka zanzibar?

2. Mt. Kilimanjaro
-The Roof of Africa, sifa zake zinafahamika kwa mapana.
-Tunaambiwa ya kuwa mlima kilimanjaro ndo mrefu zaidi Africa. Je wajua pia ni mlima Mrefu zaidi Duniani uliosisima wenyewe(bila ya kutegemezi ya safu ya milimia
)?

3. Aurora Borealis a.k.a The Northern Lights
-Natamani kuja fika sehemu ambapo nitaweza ona hizi Aurora Borealis, sehemu/nchi kama Iceland, alaska, norway etc

4. Aurora Australis A.k.a the Southern Lights
-Natamani kufika New Zealand au Australia ili nipate kuziona hizi Aurora Australis

5. The Akademik Lomonosov
-Hii ni meli ambayo ina vinu viwili vya kuzalisha umeme. Yaani ni Kinu cha Nyuklia cha kuzaliza umeme inayomilikiwa na warusi (Science, freaking science)
-Nikiiona kwa macho yangu, nitashukuru.
 
Kale kagofu kapo kwenye ule uchochoro! Sijawahi ingia pale ile nikipita naona Ka swimming pool ndani
Pazuri sana pale yaani ukilala unajiona kama Sultan Seyid Said kwenye yale magofu halafu full wazungu ukitoka koridoni unakutana na pisi za kitasha
 
Kama hujawahi kutoka nje ya nchi na unataka kuona dunia ya kwanza ikoje nenda Dubai. Gharama hazitishi na visa yake inapatikana kirahisi. Nauli kwenda na kurudi around $500, hotel siku 3/4 around $200, maana yake ukiwa na $1,000 unapata na pocket money $300.
Wewe ndio umeeleza vizuri
 
Hiyo trip ya Dubai nimeipangia mwaka ujao mwisho wa mwaka. Mwaka Huu, kuanzia 25 Desemba naanzia na Bujumbura, niivinjari Burundi, nipande kaskazini kupitia Lake Kivu hadi Goma DRC. ... Safari ya kurudi nitapitia Kigali Rwanda...

Madereva wa magari ya mizigo "Transit" kutoka Tanzania waliomo humu JF, tuwasiliane ili niunganishe nao safari ya kurudi Dar es salaam... Nitaleta mrejesho.
Road trip ya kibabe
 
Wakuu Christmas ndio hii wapi mmenda kufurahi kuona mandhari ya dunia
 
Hoteli/Lodge kwa unguja ni za kutosha from 15usd mpaka 400usd kutegemea na hitaji lako.

Eneo kama mji mkongwe kuna lodge, nje ya mji fuoni, fumba, airport, kwenye fukwe nk, kuna guest, lodge, hotel ni wewe na pesa yako mkuu.

Mkuu kuna ile lodge moja pale Fuoni ambayo ipo karibu na mtaa wanaita Jumbi last time nilipopita niliona imeboreshwa sana ipo mazingira ya kuvutia kwa nje tofauti na mara ya mwisho kuiona ilikua kama imeshachakaa kiaina.
 
Kama hujawahi kutoka nje ya nchi na unataka kuona dunia ya kwanza ikoje nenda Dubai. Gharama hazitishi na visa yake inapatikana kirahisi. Nauli kwenda na kurudi around $500, hotel siku 3/4 around $200, maana yake ukiwa na $1,000 unapata na pocket money $300.

Kwa kweli Dubai ni Best kabisa, kuko very balanced kwa wastaarabu na hata kwa watu wa vurugu.
 
Kwa kweli na ndo huwa mshangao niupatao kiasi nashindwa kuelewa wanaangalia Nini kuweka Bei kubwa kwenye accommodation

moja ya tatizo kubwa linalotutesa TZ pamoja na nchi nyingi za Africa kodi ni kubwa sana, ndio mana vitu vidogo vinakua na magharama makubwa
 
2009; Zanzibar.
nilibahatika kutembelea;
*Stone town

*National museum of zanzibar
-Hapa nilipata historia ya utawala wa kisultani ya Zanzibar mpaka mapinduzi yalipofanyika
-nilibahatika kupanda mpaka gorofa ya kwanza kuangalia mfanano wa vyumba vya masultani na familia zao
-Gorofa ya tatu tuliambiwa imefungwa kwa sababu ilikuwa "unstable"

*Slave market

*Nyumbani kwa Sultani Barghash bin Sayyid Said
-huyu mwamba alikuwa na mke mmoja na hawara 99, alijenga swimming pools 3, kila moja wanakaa mahawara 33, wakiogelea uchi, wakati huo jamaa yupo chumbani kwake, gorofa ya pili akiwaangalia kupitia dirishani, akimwona amtakaye kwa muda huo anawaambia wafanyakazi wake wanamfuata na kumpeleka room kwa jamaa.
-Alikuwa akitumia aina fulani ya "alkasusu", ambayo tourguide alipata kutaja mchanganyiko wake pale (wadada walikuwa busy kuandika).

*Christ Church
-Hapa nilipata historia ya kuuma kidogo na kusikitisha ya watumwa
-Tukaoneshwa msalaba uliotengenezwa kutoka katika tawi la mti, ambao ulipandwa/kuota katika kaburi la David Livingstone kutoka huko zambia

*Prison Island
-watumwa walifikishwa hapa kabla ya kupelekwa kuuzwa pale slave market. Kwa wagonjwa ndo ilikuwa mwisho wa safari yao maana waliuliwa na kutupwa katika shimo kubwa lililo katikati ya kambi, likizungukwa na vyumba/jela za hao watumwa
-wale watumwa wababe hapo ndo palikuwa mahala pa "kuvunja(kuwa broken spiritually), kukatishwa tamaa, kuonesha kuwa njia pekee ya kuishi ni wao kuwa watumwa"
-kuna wanyama pia kama kobe, na jamii ya digidigi(sina uhakika). pia tulionesha kobe mmoja aliekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 90 mpaka 150.
-Ufukwe wa Prison island ulikuwa murua sana

Baya pekee katika safari/utalii wa zanzibar, tulienda muda/kipindi cha mfungo. Kwa hiyo swala la chakula hasa hasa kipindi cha mchana ilikuwa issue nzito.

Tour Guide alikulisha matango pori kisawasawa kabisa, Pole sana mkuu.
 
Mkuu kuna ile lodge moja pale Fuoni ambayo ipo karibu na mtaa wanaita Jumbi last time nilipopita niliona imeboreshwa sana ipo mazingira ya kuvutia kwa nje tofauti na mara ya mwisho kuiona ilikua kama imeshachakaa kiaina.
Jumbi ipo mbele kiasi but hiyo unayosema ipo pembezoni mwa daraja la Dr. Shein, ilifanyiwa maboresho inaitwa FUONI LODGE 🤓 eneo letu la kuulia papa hilo, ukija kuanzia saa 1900 iko fully but room kwa wageni (wakulala) zinaachwa ili kuficha vifo vinavyofanyika humo ahahaaa...
 
Kwenda nchi jirani nayo ni tour wakuu kwa waliofika

Kenya
rwanda
Botswana

Watuambie kama kuna vitu vipya na bei za safari plus kila kitu ni shs ngapi?

Au ni nchi gani ya africa ni nzuri kwa kutembelea

RRONDO
 
Jumbi ipo mbele kiasi but hiyo unayosema ipo pembezoni mwa daraja la Dr. Shein, ilifanyiwa maboresho inaitwa FUONI LODGE 🤓 eneo letu la kuulia papa hilo, ukija kuanzia saa 1900 iko fully but room kwa wageni (wakulala) zinaachwa ili kuficha vifo vinavyofanyika humo ahahaaa...
Duh, kumbe ni maeneo ya watu wa hatari
 
Back
Top Bottom