Wale tunaopenda vacation, sehemu gani ya utalii Tanzania uliyofika au unatamani kufika?

Wale tunaopenda vacation, sehemu gani ya utalii Tanzania uliyofika au unatamani kufika?

Ila wadau vacation ni muhimu sana kuweka kichwa sawa.

Hata kama umepigika kiasi gani jitahidi kwenda vacation at mara moja kwa mwaka ukakae sehemu na familia hata siku mbili tatu. Inasaidia sana kutuliza kichwa na kuweka muunganiko wa familia.

Maisha mafupi haya tusiishie kuchangia harusi tu, tuweke na akiba kidogo kwenda vacation na familia hata mara moja kila mwaka. Kuna raha sana kukaa fukwe za bahari na familia zetu. Kubadilisha mazingira ya nyumbani na pia kula misosi tofauti na ya nyumbani.

Napenda vacation

tatz wtzed weng wamekarir kuw kila mwny kwnd vacation ni ana uwez but for sur ishu ni kujipang 2
 
Nataka siku tatu nitulie hotelini pekee yangu, bila kuwaza wala kufanya chochote.

Nikae tu kimyaaaa.

Maisha haya,

Ngoja najipange
 
tatz wtzed weng wamekarir kuw kila mwny kwnd vacation ni ana uwez but for sur ishu ni kujipang 2
Ingawa umeandika lugha gani sijui ila nimeelewa. Vacation zina gharama sana na zinataka maandalizi ya muda mrefu kwa mtu wa kipato cha kati. Mie nitaenda Zanzibar Desemba na familia huwezi amini nimeshaanza kuzichanga toka Januari na nimeshafikia half way kwa gharama za malazi hotel tuliyoichagua. Inakatika hela ya IST moja
Tuombeane uzima
 
namna hiyo mkuu hngera
 
Kama hujawahi kutoka nje ya nchi na unataka kuona dunia ya kwanza ikoje nenda Dubai. Gharama hazitishi na visa yake inapatikana kirahisi. Nauli kwenda na kurudi around $500, hotel siku 3/4 around $200, maana yake ukiwa na $1,000 unapata na pocket money $300.
Tatizo ni kwamba mtu akipata kazi wiki ya pili baadae amempachika mimba mtoto wa watu, majukum yameanzia hapo. Akifikiria mshahara wa miez 2 dubai na mtoto ndio kwanza yupo tumboni kichwa kinauma
 
Huu uzi unepoa sana ila kimsingi ulitakiwa kuwa active ili kutoa update kwa baadhi ya watu ambao wanatamani kufika sehemu fulani ila hawana taarifa kuhusu sehemu hizo.
 
Magoroto ni pazuri, pia gharama zake ni rafiki, papo naturally...imagine usiku mnaota Moto, kareoke, huku mkifurahia Hali nzuri ya hewa.

Ngoro ngoro pia pazuri Sana, panaleta utulivu.. na advantage nyingine pia unaweza ukapata na chance ya kupitia Manyara...

Mikumi ni cheapest zaidi, na kabla sijaenda nilikuwa nahisi hakuna wanyama Wengi, lakini kumbe ni pazuri, na gharama zake ni user friend.
Zanzibar ni breath taking...ukiwa na milioni, unaweza pata hotel nzuri ya kawaida, na ukazunguka vivutio vingi...usiku ukaenda kula urojo..
Nime wahi kwenda pia Isimila, tukuyu kuna eneo linaitwa Kaporogwe water falls, Matema beach Kyela, Bagamoyo, Na Kilimanjaro ( sikupanda mlima lakini)

Natamani kufika
Lushoto
Mwanza
Na Kigoma.
Kila mwaka sijawahi kutumia zaidi ya 1.5m Kwa gharama za utalii
Kila mwezi nasave 150,000 tuu...
Niliweka ku save zaidi nitatalii nje ya nchi...
Tufanye kazi, lakini tusisahau kuishi...
 
Wakuu ni msimu wa valentine, tusemezane kidogo wapi tutaenda kufurahi siku hii ya wapendanao
 
Ila wadau vacation ni muhimu sana kuweka kichwa sawa.

Hata kama umepigika kiasi gani jitahidi kwenda vacation at mara moja kwa mwaka ukakae sehemu na familia hata siku mbili tatu. Inasaidia sana kutuliza kichwa na kuweka muunganiko wa familia.

Maisha mafupi haya tusiishie kuchangia harusi tu, tuweke na akiba kidogo kwenda vacation na familia hata mara moja kila mwaka. Kuna raha sana kukaa fukwe za bahari na familia zetu. Kubadilisha mazingira ya nyumbani na pia kula misosi tofauti na ya nyumbani.

Napenda vacation
Ni kwa nini bei na gharama za huu utalii hazipo wazi zikajulikana kwa watu...

Sent from my 2107113SG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom