Wale wa Bwiru Boys: Tukumbushane maisha na mikasa ya Bwiru

Hahahahaha! Nimekumbuka....Mliungana na dada zetu (Advance)...Wameondoka shule asubuhi wamerudi saa 12 jioni wamechooka...Wameshindishwa nje ya ofisi ya Olenjolay...Issue pia ilikuwa kutaka chakula kizuri........Kweli jitihada zao zilisaidia, baada ya hapo tukawa twaletewa samaki mara mbili kwa wiki...siku za ubwabwa + nyama pia zikaongezeka...
 
Hahahahah.....Imagine! Yaani mwenyekiti wa kamati ulinzi na usalama ya mkoa mnamletea uvunjifu wa amani kwa sababu ya kukosa wali maharage?! Bora hata kesi ya kukosa disco na Bwiru girls......mambo ya wanafunzi sometimes very interesting!
He he he he
Ndio hivyo mkuu, na utoto unakuwemo humo humo.

Nyakati hizo siasa hazikuwa zinafahamika sana kama saa hivi.

Kwa hiyo hata chain of command inakuwa hamuwezi kuifuata pindi linapotokea tatizo.
Cha msingi shida yenu itatuliwe hata kama ni Rais wa nchi.
 
Ha ha ha ha
Ina maana ile fuso ya samaki liyokuwa inaleta sangara pale Boys ilikuwa ikitoka Boys inakunja mpaka Gilrs kushusha mzigo??

Mtushukuru sana nyie watoto wa kuwaletea neema kwa "ujinga wetu"
 
Daah, mlikua mnapewa mpaka nyama. Miaka minne ya boys nakumbuka nilikula nyama mara moja na mnofu mmoja tu tena siku ya graduation.
 
Ha ha ha ha
Ina maana ile fuso ya samaki liyokuwa inaleta sangara pale Boys ilikuwa ikitoka Boys inakunja mpaka Gilrs kushusha mzigo??

Mtushukuru sana nyie watoto wa kuwaletea neema kwa "ujinga wetu"
Ndio, ilikuwa ikishusha mzigo kwenu inaingia kwetu...kiroho safi..
Mbarikiwe kwa kujitoa kwakweli.
 
Ndio, ilikuwa ikishusha mzigo kwenu inaingia kwetu...kiroho safi..
Mbarikiwe kwa kujitoa kwakweli.
He he he he
sasa mbona hamkuomba hata siku moja ka disko ka kutupongeza kwa kazi nuri tuliyoifanya??
 
Bwiru Boys ya wakati huo ilikuwa moto! Headmaster Mkwizu akitokea Mazengo aliipaisha sana shule, combination moja tu PCM Vifaa vya kutosha na Workshops za maana! Ufaulu ukawa juu sana! Madukwa, Makula, Mlanda, Mauma, Maganga, Mwl Mazebele na kigugumizi chake alikuwa poa sana hao ni baadhi ya walimu, wengi wametangulia mbele ya haki wengine wakihama na kustaafu!
Nakumbuka mengi ya shule yangu hii! Max alikuwa mwaka mmoja nyuma yetu!
 
Bila

Bila kumsahau Tosili
 
Mwalimu nani pale Musoma Tech? Maana kuna mwalimu Muganyizi baadae akarudi Boys na kustaafia pale.

Amejenga jirani na shule kuke kijijini!

Pia Chigugu mnamkumbuka? Hahahaaa Bwiru Boys hatari sana!

Nilienda pale miaka ya 2000 katikati nikamkuta mkuu mpya anaitwa Kisuu, Mnyaturu flani, tukabadilishana namba jioni tukakutana SPAROW maeneo ya Ghana kula kilaji!

Aisee anazimeza sana. Ni mtu poa sana!

Dah nimepamisi Mwanza for real!
 
Safi sana mkuu.
Kumbe umesoma enzi za Mkwizu??

Ulikuwa electrical au Mechanical au Civil??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…