Wale wa Bwiru Boys: Tukumbushane maisha na mikasa ya Bwiru

Sio Nyemenehi ni Nyamanohi hahahahaa
 
Mwalimu Begenyezaa likuwa na macho mekundu fulani hivi anafundisha kozi za Civil Engineering hasa hasa Brickwork.

Mwalimu Muganyizi gani unayemzungumzia, maana yule aliyekuwa anafundisha Engineering Science baadaye alikuwa Second Master, tulikuwa tunamuita Bega, Pia alikuwepo Muganyizi mwingine maarufu kama mjomba, huyo alishafariki kitambo.

Chigugu Dokta namkumbuka sana na Kigugumizi chake, keshastaafu na yeye, alikuwa anaishi kwenye nyumba za mawe njia ya kama unakwenda Brweries kwa nyuma nyuma kule.

Kissuu alikuwa mtu poa sana, ila alikuwa mmoja wa waalimu makatili sana na walioiharibu ile shule.
Keshastaafu sasa hivi anakula tu pensheni yake.
 
Sio Nyemenehi ni Nyamanohi hahahahaa
Nyemenohi alikua na tabia mbaya sana, akikuta mmekaa mnapiga stori anapita nyumna kimyakimya. Akishawavuka tu anawauliza kwanini hamjamsalimia hapo mtachezea stick za kutosha.
 
Sio Nyemenehi ni Nyamanohi hahahahaa
Nyamanohi??

Tulikuwa tunamuita kifupi tu , Nyeme.

Jamaa aliwahi kuuza samani zote za ndani kwenda kuangalia kombe la Dunia Brazili nafikiri.
Ile TV tuiyokuwa tunatumia school enzi hizo ilikuwa ya kwake.

Jamaa alikuwa anakula fegi hatari.
 
Nyemenohi alikua na tabia mbaya sana, akikuta mmekaa mnapiga stori anapita nyumna kimyakimya. Akishawavuka tu anawauliza kwanini hamjamsalimia hapo mtachezea stick za kutosha.
Akikudaka lazima ukachimbe uwanja kuupanua kule walikokuwa wanakaa washangiliaji...
 
Pumbavu sana hahahahaaaa umenikumbusha class 1999 njooni hapa twende Boys! Hahaha
Ha ha ha ha
Mwaka 99??

Ulikuwa Master wangu wewe Bila shaka....
Hukuwa Bweni la Makongoro kweli wewe??
 
Wataupitia huu uzi wataona, na hivi kesho ni wikiendi
Yeah
Mara nyingi weekend JF huwa hamna nyuzi mpya.
Kutakuwa na fujo sana humu kesho.

Nilikosea timing za kuupost uzi
 
Mzee chigugu hahahaha...kisuu alipiga pesa akahamishiwa kashule ka kata kanaitwa Buigiri kapo chamwino dodoma, akaenda akahonga zile pesa akapelekwa nadhani Tosamaganga kule iringa, akastaafu saa hii anakula.pensheni yake kajenga na anaishi Moshi. Mtoto wake mkubwa Sarah alikuwa rafimi yangu mzuri tu
 
Kisuu nilikutana naye mwaka 2013 Iringa, tulikutana hotelini. Lakini nilimuona kama kawa kilema kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…