Wale wagumu wa kupiga simu tukutane hapa

Wale wagumu wa kupiga simu tukutane hapa

Ase mi nimgumu sana kupiga simu inaweza pita hata mwezi nisipige simu nyumbani au kwa wakwe,jukumu hilo analifanya wife haiwezi pita siku mbili hajapiga simu kwa ndugu zangu na zake wote

Wamesema nahisi wamechoka,
Kuna watu kweli wenye tabia kama zangu
Aisee kumbe sipo peke yangu, yaani hiyo tabia imenifanya nisihaminike kwa mpenzi wangu akawa anaona kama namsaliti
 
Mm mwenyewe huwa sipig sim japo dakik nakua nazo had znaisha muda wake
Manzi yangu huwa sianzi kumtumia sms had aanze mwenyewe na kashazoea ananijua maana akinikaushia anaweza kujikuta ndo nmeshaachana nae hvyo.

Mtu ambae sijaongea nae siku nyingi akinipigia simu huwa naona hata aibu kupokea sim yake na nikipokea dakika mbili zote naomba msamaha kuwa ni mambo tu yanaingiliana ila nisamehe sana siyo kwamba sikukumbuki, akikata simu tinamaliza miez 6 bila kumpigia sahiv wamenikaushia
 
Huwa sipendi ongea na watu, ila kazi yangu inanilazimu kuongea na mzee 1 karibu kila siku na huwa ananipigia mara nyingi ila nakuwa mvivu kupokea (yeye huwa ananiambia niachie kuweka silence kumbe ni vile naona(ga) shida kupokea


Napenda meseji zaidi kuliko kuongea, kwa ndugu wao ndo hunipigia tofauti na hapo tutakaa hata miaka 2 kimya
 
Aisee, wewe ni mimi kabisa.

Unforgettable
Tupo wengi Mkuu. Kila Mamamkwe anaponipigia simu lazima nitumie dakika tatu mpaka tano naomba msamaha kwa kutompigia simu na kuahidi kujirekebisha. Lakini bado niko vilevile. Wiki ya tatu sasa, rafiki yangu wa damu wa utotoni kapata ajali ya gari na kulazwa hospitali huko Dar. Sijawahi hata kumpigia simu wakati vocha ninayo. Nasoma tu tarifa zake kwenye group letu la WhatsApp!
 
Mimi nahisi nahitaji nafasi zaidi maana nikiwa na mawasiliano sana na watu wengine naona kama kuna kitu wananizuia katika ukuaji kiroho,Napenda kuyachunguza maisha yangu binafsi kuanzia asubuhi mpaka jioni, yani nina kazi moja ya kuchunguza kila jambo kwa maisha yangu, nikiota ndoto ni lazima niichunguze kwanini niliota vile, nikisikia amani nachunguza, nikisikia maumivu yaliyoambatana na huzuni nachunguza, katika haya yote nimegundua mimi ni mtu wa tofauti sana kwa jamii yetu, Kazi hiyo inanifanya muda mwingi kuwa peke yangu, majirani wengine hunishangaa kama vile wananionea huruma labda wanafikiru nina upweke lakini ukweli niko sawa nina AMANI,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tupo wengi Mkuu. Kila Mamamkwe anaponipigia simu lazima nitumie dakika tatu mpaka tano naomba msamaha kwa kutompigia simu na kuahidi kujirekebisha. Lakini bado niko vilevile. Wiki ya tatu sasa, rafiki yangu wa damu wa utotoni kapata ajali ya gari na kulazwa hospitali huko Dar. Sijawahi hata kumpigia simu wakati vocha ninayo. Nasoma tu tarifa zake kwenye group letu la WhatsApp!
Haipendezi mpigie leo umjulie hali
 
Mimi nahisi nahitaji nafasi zaidi maana nikiwa na mawasiliano sana na watu wengine naona kama kuna kitu wananizuia katika ukuaji kiroho,Napenda kuyachunguza maisha yangu binafsi kuanzia asubuhi mpaka jioni, yani nina kazi moja ya kuchunguza kila jambo kwa maisha yangu, nikiota ndoto ni lazima niichunguze kwanini niliota vile, nikisikia amani nachunguza, nikisikia maumivu yaliyoambatana na huzuni nachunguza, katika haya yote nimegundua mimi ni mtu wa tofauti sana kwa jamii yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kumbe ule msemo wa mganga hajigangi ni uongo
 
Back
Top Bottom