Wale wagumu wa kupiga simu tukutane hapa

Wale wagumu wa kupiga simu tukutane hapa

Kama kuna mtu hapendi simu kupiga wala kupokea kama mimi,basi akatubu!

Mimi hata nikiwa home ,nawaambia akija mtu mimi sipo.

Napenda kukaa mwenyewe,nikijisikia kuongea na mtu najua pa kuwakuta. Kazi yangu haiitaji kupigapiga simu.
 
Simu zangu mm ni za Dili na kazi tu hakuna kingine, sinaga ile tabia ya kumpigia mtu simu eti nimsalimie au nipige nae story hata mtu akinipa giant akiwa hana cha maana cha kuongea hua nakatishaga story basi poa ntakupigia kuna kazi nafanya ujue ndio imetoka hio 😣😣😣
 
Ase mi nimgumu sana kupiga simu inaweza pita hata mwezi nisipige simu nyumbani au kwa wakwe,jukumu hilo analifanya wife haiwezi pita siku mbili hajapiga simu kwa ndugu zangu na zake wote

Wamesema nahisi wamechoka,
Kuna watu kweli wenye tabia kama zangu
Wewe hutofautian na mm kabsa na nikipigiwa simu kuna muda naona kero
 
Aisee kumbe nilijua nina shida maana juzi hapa rafiki yangu aliniuliza hivi wewe huoni kama una shida simu yako ikiita basi najua tu ni demu wako maana hupigagi simu.na watu hawakupigii sasa nikamwambia nimepungukiwa nini zaidi nimepunguza kujadili watu.

Mama alishanisema sana aloo kipindi niko chuo yani sina hata 100 ila sipigi simu yeye anapiga anauliza hujaishiwa hela ndo namwambia sina imeisha sikua naweza tu kumpigia kumuomba.
Hata mwanamke wangu kanizoea tuna miaka mi2 kama nimempigia simu haizidi mara 5 dah.
Inabidi tubadilike asee sio poa wala nini.
 
Daaah! Nikajua ni jeuri yangu tu ila hili ni tatizo kubwa kwa watu wengi sana.

For sure, Mzee na Bi Mkubwa walishajua tabia yangu ya kutopiga simu ni kawaida ila nakuwa nawakumbuka sana.

Now nina almost miezi 6 sijaongea na Mzee ila Bi mkubwa kidogo ikifika mwezi 1 sijamtafuta anachukua jukumu la kunivutia waya

Sijui nifanyeje niondokane na hili tatizo na Mzee alishachukuliaga fresh tu
 
Binafsi huwa sipendi kuongea na simu hasa na mtu ambae ata taka kuleta story nyingi na siwekagi dk me ni sms na MB basi .ikitokea na dk basi zita ishia umo
 
Katika nyuzi zimewahi kunifurahisha hapa JF basi ni huu uzi. Basi mi miaka yote nikajua ni mimi peke yangu ambae siwezi kupigapiga simu! Nimefurahi sana kugundua kumbe bora mimi siwezi tu kupiga ila hua napokea, kumbe kuna watu hata kupokea hawapokei!

Mimi hata meseji tu kumtumia mtu ni lazima kuwe na ishu ya msingi, siwezi kutuma msg eti ya kusalimia. Uzuri nahisi watu walishanijua so hamna anaehangaika na mimi
 
Siwezi kabisa kuongea kwa simu. Napenda sana text kuliko kuongea. Huwa najiuliza wanao ongea kwa simu zaidi ya nusu saa huwa wanaongeaga vtu gani.
Nashukuru watu wangu wengi wameshanizoea.
Nikipigiwa au kupiga basi ni mambo ya msingi tu.
 
Back
Top Bottom