Wale wapenda mabasi ya mikoani (wanazi) tukutane hapa

Halafu niliwasahau wafanyabiashara wa miaka ile waliofuata vitu Uganda na kwenda kuuza Kariakoo au mwanza, wale wa Falcon na Taqwa, Dar to kampala,
Yes mkuu umenikumbusha ile Taqwa,Dar to Nairobi..nyuma ilibeba bango lililoandikwa ALLAN MAKABA, ule moto wake kuanzia pale kariakoo, binafsi ni mpenzi wa speed (yenye science ndani yake, all fast corners, slow corners na breaking zones ni key unapokua kwenye speed (
 

Na ukumbuke stendi ilikua kisutu, ikaja ubungo kwa sasa iko Mbezi,
 
Na ukumbuke stendi ilikua kisutu, ikaja ubungo kwa sasa iko Mbezi,
Yeah mkuu ila Kisutu ilikua zaidi kwa mabus ya kanda ya kaskazini, mabus mengi yalikua na vijistendi vyao kuzunguka maeneo ya kariakoo, mnazi mmoja mengi ya kanda ya nyanda za juu (ingawa kampuni kama kwacha ilikua na private stend yake),ubungo ilikuwa ni super place kwa stendi, ila pale mbezi ni uchafu mkubwa, pafungwe
 

Kabisa Mbezi imekaa kushoto kabisa
 
Halafu waruhusu kisheria kila kampuni ijenge stend yake Uganda, Zambia wameweza sisi tunashindwa nini?
 
Nawatafuta wale waliosafiri na Sabena Mbeya to Tabora via Chunya ambao kulala wiki ilikua kawaida kabisa hasa wakati wa mvua
Kuna kipindi nilikuwa naziona Sasse Bossa zimechoka vibaya sijui kama bado zipo, zile kona za barabara ya Chunya si mchezo, hakuna anayepeleka Basi la maana kule yote ni mikweche
 
Kuna kipindi nilikuwa naziona Sasse Bossa zimechoka vibaya sijui kama bado zipo, zile kona za barabara ya Chunya si mchezo, hakuna anayepeleka Basi la maana kule yote ni mikweche

Baada ya Sabena kuua kipindi kile akabaki Sase bossa na A.N lakini kwa sasa naona A.N anakimbiza
 
Wapo wanajikongoja naona Asante Rabi anawafuata sana
Mgamba hayupo road marangu coach, mtei na masalu wamemkazia route ya Kahama mpaka geita na route ya mwanza kule hakuna kulaza damu Asante rabi anaweka chuma nne kwa route moja, loliondo chuma 2 kwa route moja sasa wanabaki kiazi Kitamu, kaprikon bado wa Moshi Kuna nyehunge, kisesa na isamilo naona pia kashindwa kupambana.

KATARAMA n habari nyingine kwasasa chuma 2 vs chuma 8 za kampuni moja bado happy nation, kisbo, frester, Kapricon, abood wote wanaomba poo kwa KATARAMA.

Biashara n mtaji kwa kweli na kuamini kwa kidogo ulichonacho.

Mwarabu hana muda ataenda pale vingunguti Mana hawez vumilia tabu anayopewa na msukuma mmoja
 
Kapambana toka barabara ikiwa ya vumbi kaja kushindwa pazuri,hii biashara itakuwa ni ngumu mno ila ina pesa za haraka
Na mwaka Jana chuma zote zilienda bodi hata zile zilikuwa garage kafufua sa sijui imekuaje Ila Kuna ajali za kifala zilianza kumpata.

Watu wa stendi wanakwambia boss anakula posho wenyewe wanakula hesabu hutaki lete Gari stendi hutoamini macho yako.

Frey's, Kapricon chama langu kwenda wananisikitisha kwasasa
 
Ibra line nakataa
 
Vingunguti hapaendeki kirahisi bro, 95 iliyotimia na viungo vyote, retarder ,2 pedal auto opticruise gearbox , si chini ya 800 millions
Yani zile gari mbili za Katarama unaweza kuta ndo gharama ya gari hizo 8 za allys.
Heshimu sana mtu anayenunua marcopollo 95 , ana hela!!!
mpe hsehima superfeo juzi kaongeza 6 mpya , mpe heshina katarama yeye ana 2 , sauli ana moja
Heshima zaidi apewe mwamba anaitwa Nacharo, yeye marcopolo 95 imetimia viungo vyote kaamua kuipeleka Dar Tanga , nauli 16000, Mwamba haionei huruma hela yake itarudi lini na wala hana habari!
 
Katarama naona anazidi kuchukua point zake kila dakika,
 
Mpanda hakuna abood nahis una kisia tu
 
Nawakumbusha wasafiri na wamiliki wa mabasi baadhi ya milima na miteremko kama NYang’oro , kilimasera, kitonga, K nine, sekenke, mlima simba, mlima nyoka, rusunwe, kambikatoto kuibikukia namba nane, kona saba, kona za kuingia mbinga, mteremko wa kuitafuta ludewa huko, mteremko njia ya songea toka njombe kona ya shabib ilipoua abiria karibu wote, senjele ya kwanza na ya pili mbeya, Iwambi huko, kona za chunya kutoka mbeya,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…