Walikubaliana kuaona wakiwa hawana watoto kumbe mwanaume alikuwa na mtoto bila kujua, ndoa ikavunjika!

Walikubaliana kuaona wakiwa hawana watoto kumbe mwanaume alikuwa na mtoto bila kujua, ndoa ikavunjika!

Nikweli mlikuwa mnajua kila kitu..Ni uongo kusema eti Dada yenu alikuwa anazurula akakutana na mtoto anafanana na kaka yake.. uongo uongo
Na huyo mtoto alimkuta karibu na chuo alipokuwa anasoma mdogo wake.
Sio alitoka huku kwao na kwenda kuzulula mwanza
 
Habari jf ni crala kidoti tena. Hii issue ilimtokea mdogo wangu mwaka 2019 upande wa baba mkubwa wangu.
Dogo alikuwa na mchumba wa kike aliyedumu nae kwa miaka miwili kwenye uchumba. Atimaye wakafunga ndoa mwaka 2019 mwenzi wa 3. Na mkewe alimpata Na kuwa mchumba wake baada ya kuachana na mkaka mmoja hivi.

Na sababu ya kuachana na jamaa yule alikuwa na mtoto tayari aliyempata kabla ya kukutane nae. Yule binti alimchana tuu kwamba yeye awezi Olewa na mwanaume ambaye anamtoto tayari, anapenda kuwa na mwanaume ambaye anatengeneza watoto wao wenyewe. Bond ikavunjika na mdogo wangu akaanza mahusiano na huyo dada. Na walikubaliana kabisa mimi na wewe hatuna mtoto. Walienda hivyo mpaka kufunga ndoa ya kanisani. So sababu moja wapo ya ndoa kufunga ni sote hatuna watoto.

Sasa ililofika mwezi wa 7 dada wa mdogo wangu huyo ambaye wamezaliwa tumbo moja alitembelea maeneo ambayo dogo alisoma chuo kule mwanza ambapo alienda kikazi, katika kuzunguka zunguka akakutana na mdada mmoja anamtoto kafanana sana na mdogo wake ambaye amefunga ndoa mwezi wa 3, na akiangalia yale maeneo mdogo wake ndipo alipokuwa anaishi na ni karibu na chuo.

Sasa dada mtu baada ya mshituko akaamua kwenda kwa Dada mwenye mtoto ilikupata data, akamuuliza huyu mtoto Baba yake yupo wapi, dada yule akamjibu kuwa kuwa alikuwa anasoma chuoni hapa. Alinipa mimba kipindi amemaliza chuo hapa sikukutanane tena baada ya kuondoka. Dada akaamini ni mdogo wake kwa sababu kafanana naye kabisa. Akamwambia unaweza kunitajia jina akamtajia jina la mwanzo, likawa jina hilohilo dada akachukua simu na kumuonyesha picha ya kaka yake , dada mwenye mtoto akasema ndio huyo huyo.

Dada mtu bila kuchelewa akapiga simu home na kuwaeleza kila kitu. Baada ya siku kumaliza kazi yake akaenda kwao na kuwaambia kila kitu na mama akaamua kuwasiliana na Dada yule na kuongea nae. Walionyesha picha na dogo kweli walifanana hivyo hivyo.

Sasa familia wakaamua kumwambia dogo kuwa unajua mtoto sehemu flani , dogo akasema yeye hana mtoto kabisa. Dada mtu akaamua kumwambia kila kitu, dogo alipata mshangao sana. Maana anaelewa makubaliano na mkewe.

Dada za jamaa wakawa wanang'ang'ania mtoto haye humu ili wamjue vizuri vizuri mtoto. Baba mtu akasema mambo haya tufanye kwa utaratibu msikurupuke maana kijana mdogo wenu ameshaoa ana mke , mama na dada zake walimpenda mtoto yule wakawa wanataka aje home. Huku kaka yao anazuia, Mwishowe walimtumia nauli dada yule aje home.

Sasa kaka yao katika kuangaika kuangaika mkewe wake akajua kuna kitu hapa kwani alimuuliza mbona kama huko sawa shida ni nini, anakwepa kumwambia simu zilikuwa nyingi sana anapigiwa na dada zake aje home coz dogo kashafika na unaweza usimwambie mkeo tutatafuta namana ya kumwambia mkeo usijali.

Baada ha simu kuwa nyingi na maongezi mkewe si akasikia bwana mazungumzo. Case ikawa kubwa sana.

Kwa kifupi mkewe aliamini familia ilishirikiana kumficha yeye, kuhusu kaka yao kuwa na mtoto. Kwa nzia siku ile ndoa ilikosa amani kabisa, yule Dada alikuwa analia kama kafiwa na mume vile tena mume aliyemtegemea. Daa niliona huruma sana nikikumbuka.

Baba yao akasema niliwaambia case kama hizi inahitaji kuwa na hekima kuzisuruhisha.

Dada zake kama mawifi si unajua wakaanza kusema huyu ni damu yetu atuwezi itupa.

Sasa kuweka sawa ile kesi wazazi wa dogo wakamwambia kuwa wewe endelea na ndoa yenu mtoto hatakuja kuishi kwenye nyumba yenu.
Ila yule dada still aliamini kuwa familia ilimficha kuhusu ilo.
Na aliwaambia hana imani tena na familia yenu na hata kwa mume wake, walijaribu kumshawishi hata kutumia wazazi wake na viongozi wa dini na walimwambia kuwa unandoa ya kanisani. Lakini still alikataa katakata, yule dada alikuwa analia mpaka huruma.

Wazazi wake walimshauri basi aendela na ndoa yenu tuu haina shida mtoto hana shida yoyote ila dada alisema hawezi ishi na mtu ambaye kampa
maumivu makali kwenye maisha yake. Na dada yule kutokana na maumivu na vilio mimba ilitoka ilikuwa na 2 month hivi, kutokana na situation ile.

Mwishowe dogo aligombana sana dada yake akiona kama kamwalibia ndoa yake , tena ngumi kama ngumi na maneno, mpaka leo hawapatani na dada yake. Dada mtu alijaribu kuomba msamaha ila wala.
Kwa kifupi ndoa ilivunjika.

Kama ungekuwa wewe mtu mzima case kama hii unaisove vipi.
Una ishuruhisha kivipi karibuni jamani.
Tuambie kwanza, yule kijana umempa mbususu?
 
Ndoa siku hizi zinavunjika sana me na mshkaji wangu mimemsimamia ndoa ya mwaka juzi dec na mwaka huu Jan imevunjika
Na walikuwa uchumba miaka 10
 
😂😂😂Kwamba amkatae mtoto kisa makubalino yao ya kitoto kitoto?
Najua ungekuwa wewe wala usinge vunja ndoa eti kisa mumeo ana mtoto na hakukuambia. Huyo binti ana utoto mwingi
 
Mwanamke ana matatizo ya akili, lakn pia wif zake wana pupa sana
 
Hats ukiikana si inabaki kuwa damu yako tu, so kuna tatizo gani ukiikana kwa lengo la kuokoa ndoa?
Halafu ikitokea huyo mke uzao unagoma unahangaika kuitafuta damu uliyoikana!
 
Najua ungekuwa wewe wala usinge vunja ndoa eti kisa mumeo ana mtoto na hakukuambia. Huyo binti ana utoto mwingi
Siwezi kufanya huo ujinga,, navunjaje ndoa kwa mtoto mkubwa kuzidi mahusiano

Inahitaji akili ya kipuuzi aisee
 
Halafu ikitokea huyo mke uzao unagoma unahangaika kuitafuta damu uliyoikana!
Uhusiano wa damu haupotei kwa mtu kuukana, biological atabaki kuwa baba wa mtoto. Kukana ni kitendo cha kumtaa kwa maneno kuwa si mwanae. Ila mwenye akili anaweza kumkataa na kisha akamhudumia kama mwanawe, mtoto mwenyewe ataona kuwa baba alichofanya pale ilukuwa ni kuishi kwa akili na wanawake. Unadanganya pasipo kumaanisha
 
Tena chekechea za zamani. Siku hizi wana akili na hawawezi kuamini. Uvamie tu mtu njiani eti huyu mtoto kafanana na fulani na uamue kufuatilia! Tena mtoto mdogo! Umri ambao unaweza kuhisi ni mtu anapokuwa mtu mzima. Kwenye age ya utoto siyo rahisi uone mtoto ambae hata humjui eti anafanana na ndugu yako na uchukuwe uamuzi wa kupeleleza!
Damu yako hata ikiwa mbali kuna mazingira itarudi katika namna usiyo tarajia, njia za Mungu hazichunguziki
 
Back
Top Bottom