Walimu acheni kuwafundisha watoto wetu mabongo fleva kwenye mahafali za shule

Walimu acheni kuwafundisha watoto wetu mabongo fleva kwenye mahafali za shule

Hatuwezi kuwalaumu walimu moja kwa moja ingawaje wanachangia sana kutengeneza future ya mtoto almost kwa 60%, including morally and spiritually.

Changamoto kubwa ni kwa walimu kizazi kipya na hawa watoto wetu tunaolea hovyo hovyo.
 
Kama ni mziki wenye maadili hakuna shida ila kwa nyimbo za matusi sio sawa.
unajua sisi ndo tunatafsiri mziki vibaya ndugu na kwa kizazi hiki ambabo hakiambiliki cha kuiga kila kitu tutafka tumechoka. Lakn tukirud nyuma wazungu mtu anaimba matusi tena ya nguoni lakn huku ndo kwanza tunaushbikia mziki wao mwanzo mwisho. Sasa kwa hili tusilaumu walimu bali tulaumu teknologia. Kila mtu ndan ana tv kama huna tv simu kubwa unayo mda upo nyumban watoto ni walokole lakn ngoja utoke sasa nyumba inageuka ya mazombie. Hapa la msingi ni kumuomba mungu na mababu waingilie kati.
 
Ila wakiwa nyumbani ni mwendo wa tamthilia tuu akina jua kali na kombolela?
😂😂 Umenikumbusha nilivyomtia vibao vya haja mke wangu sababu nilimtuma aniletee kiberiti ili ni home sigara yangu akaniambia hadi tamthiliya ya BONDITA iishe.
 
Haya mambo ya magruduesheni shuleni tulishaachana nayo kitambo sana kunako shule moja. Hatunaga swaga hizi, mwanafunzi akishahitimu imetoka hiyo, hatuna mahafali sisi, hatusumbui wazazi na wanafunzi kutoa michango ya graduation. Cha ajabu siku hizi eti mtoto anafanyiwa mahafali nyumbani kwao. Watoto wanaimbishwa nyimbo za ajabu ajabu na mitindo ya kihuni kucheza
 
Kama una huakika kua mwanao akimaliza kusoma atakua nani kwakweli sio jambo jema kuchezeshwa na kuimbishwa..ila tambua walimu wanatoa fulsa kwa wanafunz kuonyesha au kuwapa uzoefu wa utafutaj nje na masomm
 
Asilimia kubwa ya sisi wazazi tunaojitambua haturuhusu watoto waangalie au wasikilize nyimbo za bongo fleva sababu nyingi hazina maadili.

Ila cha kushangaza unaenda kwenye mahafali unakuta mtoto anakata viuno na kuimba mabongo fleva eti ndio burudani siku ya mahafali.Manyimbo yenyewe mnayowafundisha unakuta yana matusi.

Kama ni kuimba waimbe wenyewe nyimbo zao walizofundishwa za maadili lakini sio kuwakaririsha sijui saparapa na mabongo fleva.

Content za kisomi zipo nyingi sana kwa ajili ya burudani na sio hayo mabongo fleva.
Ukitaka kujua hawajifunzi shuleni angalia vibe lao na namna wanavyoziimba nukta kwa nukta halafu jiulize kama zipo kwenye mtaala wa elimu. Kama hazipo hawawezi zikariri ndani ya siku moja ya graduation.
 
Utandawazi 90%, everything is everywhere hata kama nyumbani hakipo. Kwa hiyo ni ngumu sana kumzuia mtoto labda awe anajitambua.
 
Mtoto yake katuni tu

Ila Azam na dstv hizo tamthilia zimeharibu kizaz hichi nyimbo za zuchu ndo usiseme hata kama kwako hasikilizi hizo nyimbo shule anawasikia wenzake wakiimba
 
Hata hao marafiki wa mwanao wanahusika pakubwa kwenye hizo nyimbo n bc tuu mzigo unawabebesha waalimu
 
Kuna walimu siku hizi wana record content wakicheza hizo nyimbo na watoto darasani hilo limekaaje
 
Back
Top Bottom