Rorscharch
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 878
- 2,014
Kwa kizazi hiki cha kidigitali, kama mwalimu unaendelea kufikiri kwa mtazamo wa kianalogia, ni wazi kwamba wanafunzi wako watakudharau sana. Fikiria, unawafundisha kuwa kuna sayari tisa, lakini wao wakigoogle wenyewe wanagundua kuwa zipo zaidi ya 1,000. Unategemea watachukulia masomo yako kwa uzito gani? Kwanini usijitahidi kuendana na wakati na kuepuka kuonekana kilaza?
Hivi unajua kwamba baadhi ya wanafunzi wako tayari wanaitumia ChatGPT na teknolojia nyingine za kisasa? Lakini wewe bado unashindwa kujiimarisha na kujifunza mbinu mpya za kufundisha? Kwanini wasikuone kama mfano wa kale kila unapojongea ubaoni? Siku hizi, watoto hawakusikilizi kwasababu tu ya mamlaka yako au ukali, wanakusikiliza kwa sababu kile unachowafundisha kinagusa akili na maslahi yao.
Ninakumbuka mfano mmoja wa mtoto wa mjomba wangu, ambaye amekuwa akilelewa na baba yake msomi mwenye upendo mkubwa wa vitabu. Mtoto huyu, sasa yupo darasa la saba, lakini ana shauku kubwa ya kusoma vitabu vya astronomia. Nilimfanyia majaribio madogo kuhusu mada tofauti za anga za juu – ambayo nilikuwa nimegugulisha – na kwa mshangao wangu, kila kitu alikuwa anakielewa kwa undani. Mtoto huyu, aliyekuzwa katika mazingira ya elimu ya nyumbani, anaonekana kuwa mbele zaidi kuliko walimu wengi wanaomfundisha shule.
Sasa wewe unapeleka watoto English Medium, wanajifunza kwa kukariri tu, wakati msingi wa elimu bora huanzia nyumbani. Unajiitaje mzazi wa mtoto msomi ilhali huna hata shelf moja ya vitabu nyumbani? Ni wakati wa kubadilika – si kwa walimu tu bali pia kwa wazazi! Tukumbuke, elimu bora huanzia katika mazingira tunayowapa watoto wetu. Tubadilike!