Elimu bora ina athiriwa na ushindani wa mitihani. Wanafunzi wanataka wafaulu ilibwa songe mbele, Mwalimu anataka aonekane amefaulisha, anapaswa kumaliza mada zote kwa wakati. Shule zinataka jina kwa kukuza ufaulu na mnyororo unaendelea.
Ni mkanganyiko wa kufamtu: sera ya elimu itungwe na wizara husika, mtaala wa kufundishia utungwe na TIE, kitabu cha kufundishia kitoke TIE , anae taini na kutunga mitihani NECTA: wanatoa format, watunga mitihani na wanasaisha mitihani, na mwalimu kazi yake: kufundisha TIE wanavyoelekeza, kufanyisha mazoezi kutosha ili wafaulu kama NECTA wanavyotaka.
Maabara zipo lakini hazitumiki kufundishia, walimu hawana muda huo; zinatumika tu kwa ajili ya madarasa ya mitihani. Miongozo na maelekezo kibao inayoua ubunifu wa mwalimu darasani, watoto wanapewa elimu kavu; unafundishwa kitakachotoka kwenye ntihani wako wa mwisho.
Katika elimu hii inayopimwa kwa makaratasi inaleta ugumu wa mwalimu katika kuonesha ubunifu unaoacha elimu kwa mwanafunzi. Elimu hii imekuwa kama mechi za mtoano, matokeo yanazingatiwa zaidi kuliko michakato