nafanya kazi wilaya ya rorya mara napenda kwenda musoma mjini mwalim mwenye hitaji tuwdiliane
DUUUUUUUH
Kasi ya mauaji Musoma yaongezeka T
Details
Imechapishwa Ijumaa, 08 Februari
2013 22:03
Imeandikwa na Erasto Mkumbange,
Butiama Imesomwa mara: 55 KIJANA mmoja aliyetambulika kwa jina la Magere.
Masatu Mkazi wa Mtaa wa Nyakato,
Wilaya ya Musoma ameuawa kisha
kutupwa mtoni. Katika tukio hilo
wanajeshi waliingilia kati na kufanikiwa kudhibiti maafa zaidi baada ya nyumba moja ya mtuhumiwa wa mauaji hayo kuchomwa moto.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo la
Februari 4 mwaka huu katika kijiji cha
Etaro wilayani humo, walisema kuwa siku ya tukio marehemu aligongana na
pikipiki ambapo marehemu aliamua
kumlipa fedha aliyegongana naye lakini balozi wa eneo la tukio
alipelekewa pikipiki ya marehemu kwa
ajili ya kuihifadhi. Baada ya tukio kweli pikipiki ilichukuliwa na kupelekwa kwa balozi wakati wanakwenda kuna vijana wawili walikuwa wakifuatilia kwa nyuma, na baada ya hapo marehemu
hakuonekana tena hadi jana alipoonekana amekufa na yupo ndani
ya mto, alisema shuhuda aliyekataa
kutaja jina lake.
Baada ya waendesha pikipiki wa Wilaya ya Musoma kupata taarifa kwa kuuawa kwa mwenzao walikwenda na kuvamia kijiji hicho kwa kuwapiga baadhi ya wananchi na balozi ambaye alikuwa amehifadhi pikipiki hiyo kisha kumtaja mmoja wa wauaji hao kuwa ni Koti Magee mkazi wa kijiji hicho.
Waendesha pikipiki hao walikwenda hadi kwa mtuhumiwa huyo na walimkuta lakini alifanikiwa
kuwatoroka kisha kukimbilia ziwani na
kujitosa kwenye maji kuogelea ikiwa
ndio pona yake.
Baada ya kumkosa vijana hao walirudi nyumbani anapoishi kijana huyo ambaye anaishi na baba yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Magee Saganda kisha kuitia moto nyumba moja na kuteketea kabisa.
Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania waliwahi kufika
katika eneo la tukio na kuzuia uchomaji moto wa nyumba zingine.
Jeshi la polisi baada ya kufika lilichukua mwili wa marehemu na Balozi wa eneo hilo Peter Mabojano na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kwa
ajili ya mahojiano zaidi.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika. Hospitali ya Mkoa huo na
umehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhia maiti kwa ajili ya taratibu
za mazishi. Tukio hili ni la tano kutokea katika wilaya ya Butiama kuanzia Novemba mwaka jana hadi
Februari mwaka huu.
Matukio hayo ni pamoja na la Desemba 21, mwaka huu saa 5:30 usiku Tabu Makanya (68) Mkazi wa Kijiji cha Kwikuba alichinjwa lakini watuhumiwa wakiwa katika harakati ya kuondoka na kichwa chake waliwahiwa na wananchi kisha kukitupa.
Tukio lingine lilitokea Desemba 2, Blandina Peru alichinjwa
na kuchukuliwa damu yake tu na Sabina Mkireri wa kijiji cha Kabegi, alichinjwa na kuondoka na kichwa
chake. Aidha kijana aliyetambuliwa
kwa jina la Thomas Majengo (23-28)
Mkazi wa Kiara, Musoma Mjini
alichinjwa na kunyang'anywa pikipiki.