Kama kweli mngekuwa na Mshahara mzuri msingetolea macho mambo ya sensa za 30k kwa siku.
Tumesikia kuna vijana wameuana huko Geita, kisa sjui cheo gani labda kuwa second master....
Nje ya mshahara hakuna allowance yoyote, unaishi Dodoma, mara unapangiwa ileje vijijini kufika shuleni unavuka mto na mtumbwi, Nanasi utakula siku mshahara ukitoka, unaona mwalimu katoka mjini kabeba matunda sasa.
Yaani ishafikia hatua mwalimu anaonekana tu kwa macho hata kabla hujamuuliza.
Headmaster ni Mungu mtu akiongea wengine wanatetemeka..
Mnakosa exposure kiasi kwamba gari ikiingia eneo la shule watu wanaanza kutetemeka....wanawaogopa watu wa halmashauri kama Miungu yao.
CWT inawanyonya kama kupe na wapo tu.
Mwalimu ukimwambia Nje ya ualimu anaweza akafanya kazi nyingine anakwambia "Inawezekanaje"? Yeye aanachojua ni kufundisha tu..
Kuna mahali mpywayungu anawagusa na mnaujua ukweli