Walimu Mei mosi imekaribia, andaeni mabango ya maandamano ya Amani

Walimu Mei mosi imekaribia, andaeni mabango ya maandamano ya Amani

Halafu mkuu wewe hao walimu unaosema wana shida ni wa wapi?
Mbona mimi na wenzangu ninaowajua tuna maisha fresh kabisa? Tuna maisha yanayoridhisha kabisa.
Mnapewa haki zenu? Yani walimu ahsee [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwanini uwe muoga kwenye kudai haki zako? Ivi unajua uoga unafedhehesha zaidi ya umasikini. Basi niwaambie tu mimi nitawadharau nasitawasalimia mpaka mtakapoandamana kudai haki zenu

Walimu wengi wana miaka zaidi ya kumi kazini ila wakiomba uhamisho hawapewi na vigezo wanavyo, uhamisho wa kubadilisha pia ni mbinde majina yanatoka ila vibali havitoki, una Miaka kumi na mbili ila umepanda daraja Mara moja tu, pesa yako ya kujikimu mpaka Leo hujamaliziwa unapewa nusu nusu, mshahara wako wa kwanza mpaka Leo hujalipwa unadai malimbikizo hata mfuko wa shangazi kaja unajaa, mnakaa kwenye magofu, Mnaishi Kwa kutukanwa, mnapigwa biti na mkuu wa shule mnapwaya, Mnaishi Kwa huzuni kama yatima, mna madeni yasiyoisha, mishahara yenu niyamiaka kumi nyuma Dunia ya sasa kupewa laki tano ni matusi, hamna posho yoyote, hata kununua pikipiki tu mpaka ukope maana kusave million Tatu na Familia uliyonayo haiwezekani.

Walimu walimu please Mei mosi nataka muandamane, nataka walimu mdai haki zenu. Vinginevyo nitawadharau mpaka kufa mmekuwa waoga kama ngiri jamani.
Halafu pendaneni muwe kitu kimoja hakuna mapinduzi bila umoja. Mkuu wa shule akileta ukuda mpigeni spana za kutosha kwenye vikao vyenu mpaka ajihisi kajinyea

Acheni woga hakuna wakuwakomboa zaidi ya kujikomboa nyinyi wenyewe, lazima ifike wakati mseme enough is enough
We umeshaandamana ktk lipi, we haki zako zote unapata?
 
Usituchoshe maana sisi tunaishi Kwa uzalendo Kwa kufuata ideology ya mwalimu Nyerere. Kama Kuna mwalimu kaja kutafuta utajiri kupitia kwenye uwalimu basi nashauri aondoke hayupo sehemu sahihi

Mbona unatunanga sana kwani vipi weweeee hebu tuache haloooo. Walimu wote tupo pamoja na serikali maana bila mama Samia mimi watoto wangu hawawezi kula kwasababu yeye ndio ananipa mshahara. Huwezi mpangia boss wako kiasi gani cha pesa akulipe

Kwa mwalimu ambae anaona anaonewa aondoke sisi hatuna shida na utajiri. Kama unaona laki tano ndogo jaribu kumpa ambae hana kazi kama ataona ndogo
 
Mnapewa haki zenu? Yani walimu ahsee [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Haki za nini ?
Tunalipwa mshahara kwa wakati. Tukitaka mkopo tunapata. Yaani wafanyakazi wa taasisi nyingine na sisi hamna tofauti sasa haki gani tena?

Mshahara unatosha kuendesha maisha. Na hapa nataka nikasome Master's Degree soon.
 
Back
Top Bottom