Kwanini uwe muoga kwenye kudai haki zako? Ivi unajua uoga unafedhehesha zaidi ya umasikini. Basi niwaambie tu mimi nitawadharau nasitawasalimia mpaka mtakapoandamana kudai haki zenu
Walimu wengi wana miaka zaidi ya kumi kazini ila wakiomba uhamisho hawapewi na vigezo wanavyo, uhamisho wa kubadilisha pia ni mbinde majina yanatoka ila vibali havitoki, una Miaka kumi na mbili ila umepanda daraja Mara moja tu, pesa yako ya kujikimu mpaka Leo hujamaliziwa unapewa nusu nusu, mshahara wako wa kwanza mpaka Leo hujalipwa unadai malimbikizo hata mfuko wa shangazi kaja unajaa, mnakaa kwenye magofu, Mnaishi Kwa kutukanwa, mnapigwa biti na mkuu wa shule mnapwaya, Mnaishi Kwa huzuni kama yatima, mna madeni yasiyoisha, mishahara yenu niyamiaka kumi nyuma Dunia ya sasa kupewa laki tano ni matusi, hamna posho yoyote, hata kununua pikipiki tu mpaka ukope maana kusave million Tatu na Familia uliyonayo haiwezekani.
Walimu walimu please Mei mosi nataka muandamane, nataka walimu mdai haki zenu. Vinginevyo nitawadharau mpaka kufa mmekuwa waoga kama ngiri jamani.
Halafu pendaneni muwe kitu kimoja hakuna mapinduzi bila umoja. Mkuu wa shule akileta ukuda mpigeni spana za kutosha kwenye vikao vyenu mpaka ajihisi kajinyea
Acheni woga hakuna wakuwakomboa zaidi ya kujikomboa nyinyi wenyewe, lazima ifike wakati mseme enough is enough