Walimu msipokuwa makini mwaka huu, mtakwisha!

Walimu msipokuwa makini mwaka huu, mtakwisha!

Mtanzania mmoja mwizi wa mbolea unahitimisha kuwa watanzania ni wezi wa mbolea!
Akili ya wapi hii?
Ndivyo ulivyofundishwa na walimu wako?
Samaki mmoja akioza wote wameoza. Hukuebda shule nini? Huko shuleni umeenda kusomea ujinga? Cc FaizaFoxy
 
Acheni ujinga! Mmesahau kipindi Cha likizo ya Corona (miezi miwili).
Wazazi waliona kero kukaa na watoto muda mrefu nyumbani.

If education is expensive try ignorance.
Mfano wako hausadifu mada iliyopo hewani
 
We mwenyewe unaonesha ni kiaza +, hueleweki umeandika nini, umetupotezea muda tu kusoma andiko kuubwa ndani hamna kitu.

Inaonesha una chuki kubwa na walimu, bila hoja za msingi. Walioua, waliobaka, wezi na wakosaji wengine wote waalimu? Panua fikra zako kidogo
Watu making wote wameelewa andiko.Tatizo walimu mnajiona mko "exceptional" kumbe mpo wa kila aina negatively kama alivyosema mtoa post.
 
Huna hoja mtoa mada,unaonekana elimu yako haijakusaidia,na inawezekana una watoto wajinga,wapumbavu kama wewe,bila huyo mwalimu unayemwita kilaza hata huko kuandika usingeweza hata kidogo,,,jaribu kutumia akili yako vizuri kuondokana na negative attitude dhidi ya watu wengine ama makundi mengine,,,kama wewe Mungu amekujalia kipato cha kutokwenda kwa hao kausha damu mind your business cause hata hao wanaoenda kwa hao kausha damu hawajawahi kuja mlangoni kwako kukuomba chochote na kingine usipende sana kujumuisha kosa la watu watatu kuwa kosa la watu 500 ni ujinga kiwango la lami
Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza

Walimu wanne wa shule za msingi zilizopo Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza pamoja na mfanyabiashara mmoja mkazi wa Wilaya ya Nyamagana wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka za watumishi wa serikali ili kupata mikopo katika taasisi mbalimbali za kifedha.

Akizungumza jijini hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa ameeleza kuwa tukio hilo liliripotiwa kituo cha Polisi Misungwi Januari 4,2024 baada ya kugundua kwamba baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wamesitishiwa makato ya mikopo yao wakati bado hawajamaliza kulipa madeni yao.

Baada ya ufuatiliaji Jeshi la Polisi liliweza kubaini kuwa nyaraka za kusitisha mikopo hiyo zilighushiwa na watumishi hao na kwenda kuomba mikopo mipya kwenye taasisi nyingine huku wakijua bado wanadaiwa marejesho kwenye taasisi walizokopa awali.

Watuhumiwa waliopanga na kuratibu njama za kughushi nyaraka kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia isiyo halali ni Majaliwa Philipo Mwaikambo,(34),mfanyabiashara na mkazi wa Nera Kata ya Isamilo ambaye ni mtuhumiwa sugu wa kughushi nyaraka.

Wengine ni Magreth Michael Simba (42), Mwalimu wa shule ya msingi Ntende Wilaya ya Misungwi,Mariam Ngwile (48),Mwalimu wa shule ya msingi Usagara Wilaya ya Misungwi, Beatus Nyombi,(53),Mwalimu wa shule ya msingi Mbalama Wilaya ya Misungwi na Jitashika Ezekiel Nchemba,(42),Mwalimu wa shule ya msingi Ntende Wilaya ya Misungwi.
 
Nitajie mmoja kutoka makundi yafuatayo unayedhani ni intelligent kuliko mwalimu:
1.TISS
2.Polisi
3.JWTZ
4.Wanasiasa
5.Madaktari wa afya
6.Wansheria
7.Wahandisi.
NB.Taja jina la mtu husika kutoka kundi moja wapo aliye bright kuliko mwalimu.
Ili nikueleze ukweli.
Wanasiasa mkuu.
 
Back
Top Bottom