Walimu msipokuwa makini mwaka huu, mtakwisha!

Mtanzania mmoja mwizi wa mbolea unahitimisha kuwa watanzania ni wezi wa mbolea!
Akili ya wapi hii?
Ndivyo ulivyofundishwa na walimu wako?
Samaki mmoja akioza wote wameoza. Hukuebda shule nini? Huko shuleni umeenda kusomea ujinga? Cc FaizaFoxy
 
Acheni ujinga! Mmesahau kipindi Cha likizo ya Corona (miezi miwili).
Wazazi waliona kero kukaa na watoto muda mrefu nyumbani.

If education is expensive try ignorance.
Mfano wako hausadifu mada iliyopo hewani
 
Watu making wote wameelewa andiko.Tatizo walimu mnajiona mko "exceptional" kumbe mpo wa kila aina negatively kama alivyosema mtoa post.
 
Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza

Walimu wanne wa shule za msingi zilizopo Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza pamoja na mfanyabiashara mmoja mkazi wa Wilaya ya Nyamagana wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka za watumishi wa serikali ili kupata mikopo katika taasisi mbalimbali za kifedha.

Akizungumza jijini hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa ameeleza kuwa tukio hilo liliripotiwa kituo cha Polisi Misungwi Januari 4,2024 baada ya kugundua kwamba baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi wamesitishiwa makato ya mikopo yao wakati bado hawajamaliza kulipa madeni yao.

Baada ya ufuatiliaji Jeshi la Polisi liliweza kubaini kuwa nyaraka za kusitisha mikopo hiyo zilighushiwa na watumishi hao na kwenda kuomba mikopo mipya kwenye taasisi nyingine huku wakijua bado wanadaiwa marejesho kwenye taasisi walizokopa awali.

Watuhumiwa waliopanga na kuratibu njama za kughushi nyaraka kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia isiyo halali ni Majaliwa Philipo Mwaikambo,(34),mfanyabiashara na mkazi wa Nera Kata ya Isamilo ambaye ni mtuhumiwa sugu wa kughushi nyaraka.

Wengine ni Magreth Michael Simba (42), Mwalimu wa shule ya msingi Ntende Wilaya ya Misungwi,Mariam Ngwile (48),Mwalimu wa shule ya msingi Usagara Wilaya ya Misungwi, Beatus Nyombi,(53),Mwalimu wa shule ya msingi Mbalama Wilaya ya Misungwi na Jitashika Ezekiel Nchemba,(42),Mwalimu wa shule ya msingi Ntende Wilaya ya Misungwi.
 
Wanasiasa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…