kaligopelelo
JF-Expert Member
- Jun 20, 2013
- 2,832
- 4,070
Zamani nilikuwa najua kuwa walimu ni kioo Cha jamii,kumbe nilikuwa najidanganya huenda ni kwasababu nilikuwa mtoto kipindi hicho au kwasababu walikuwa watu wa karibu yangu kwasababu nilikuwa mwanafunzi na niliwachukulia kama watu waliofanikiwa zaidi katika jamii.
Leo nashuhudia mengi kutoka kwao mpaka napingana na mtazamo wangu wa zamani. Kumbe walimu wengi wao ni wahuni kuliko vile nilivyokuwa nadhania.
Juzi juzi tu hapa walimu wameuana kugombania madaraka,aibu sana hii. Mara walimu utasikia wamekutwa na kashfa ya wizi wa mitihani wengine wameiba fedha za miradi. Kuna wengine wamekutwa na hatia Kwa makosa ya kuwaweka mimba wanafunzi wao.
Serikali imewapa vishikwambi lakini wengi wao wanavitumia kubetia. Wengine wameshaviwekea poni vilabuni Kwa kushindwa kulipa bili za pombe chafu walizokuwa wanakopa.
Tukija Kwa askari polisi nao hali kadhalika. Wengi wao wanavuta bange na kutumia vilevi vikali sana. Wameharibu maisha yao kwa kuendekeza anasa.
Askari polisi mnakula rushwa bila haya. Mnatumika na wanasiasa kama vile mfugaji anavyotumia mbwa kulinda mifugo yake. Mpo kulinda masilahi ya wanasiasa wenyewe mkiendelea kuvaa sare zenye viraka na viatu vinavyocheka.
Jirekebisheni mnatia aibu.