HABARI YA WANABODI?
Kuna huu upumbavu, umenikera. Hebu tusaidiane kuutatua.
NI JUU YA WAALIMU MALAYA WA BUTIMBA SEKONDARI-MWANZA
....Mwalimu mwanzalima na mwalimu paul....(JELA INAWAITA)
Mwalimu wa Butimba sekondari wiki hii alitaka kumbaka mwanafunzi ila Mungu saidia aliweza kumponyoka na kukimbia.
Mwanafunzi huyo wa kike sketi yake ilichanika, ilikuwa masomo ya saa tisa hivi.
Mwanafunzi alienda moja kwa moja kwa mama yake na kumjuza juu ya tukio hili. Mzazi alitoa taarifa kwa kiongozi mmoja wa chama na kiongozi wa chama akaijuza serikali na serikali ikamtuma afisa elimu wa wilaya ya Nyamagana kutatua mgogoro huo.
Mwalimu aliohijwa ila alikana kabisa kuhusika na tukio hilo.
Kikao cha mkuu wa shule na walimu pia hakikuzaa matunda, mwalimu bado alikana kata kata kuhusika na tukio hilo.
Mkuu mpya wa shule alimuita mzazi wa binti huyo wakaongea nae kwa kumpoza ili suala liishe, na hakika kwa mzazi na mwanafunzi ni kama limeisha.
Timu ya afisa elimu wamesema watapeleleza zaidi kuufahamu ukweli.
HALI YA SASA YA MWALIMU ALIYETAKA KUBAKA
Tangu timu ya afisa elimu kusema watalifanyia uchunguzi, mwalimu ameonekana akiongea na baadhi ya wanafunzi wa kike akiwa na sura ya hofu kana kwamba kuna kitu anataka kuficha.
TUKIO HILI LILITOKEAJE?
Kwa ufupi walimu hao wawili ofisi yao ni maabara ambayo ina magrill na mapaazia mazito.
Mwanafunzi huyu aliitwa na mwalimu huyo kuchukua mtihani wake.
Mwanafunzi huyo alienda, mashuhuda wawili wanazidi kusimlia.
Mwanafunzi alipoingia, pazia lilishushwa. Gafla wakaskia kelele kama ugomvi, niache, niache. Dakika sio nyingi, vitu kama vinadondoka ndani, ndipo mwanafunzi akatoka akikimbia huku kashikilia sketi imechanika. Moja kwa moja akaenda nyumbani
Binti huyu anasema mwalimu huyu amekuwa akimtongoza tangu kidato cha kwanza.
MWALIMU MWINGINE
Mwalimu mwingine huyu, anaekaa maabara. Mwenye sifa kama mwalimu wa kwanza. Huwaita wanafunzi na kuwawekea mziki kwenye smart phone na wanafunzi kuanza kucheza.
Mara kadhaa huwashika makalio na matiti na baadhi yao huwapa miadi wakutane siku za Jumamosi au Jumapili.
MHANGA MMOJA ANASIMULIA
Mwanafunzi mmoja wa kike, form one alichukizwa na kitendo cha mwalimu huyu, alimshika matiti na makalio. Alienda na kusema kwa mzazi.
Mzazi alilipeleka kwa mkuu wa shule, kikao kiliwekwa na mwalimu alionywa ingawaje hakukubali kosa.
Mwanafunzi huyu kaandamwa sana na walimu hawa wawili kwa manyanyaso ya kijinsia hadi anaomba ahamishwe shule. Ni matusi kwake na kejeli . Kwamba, umeshtaki imesaidia nini? Kwani hujawai kufanya?
Inauma sana.
YUPO MWALIMU ALIWAHI KUOA MWANAFUNZI BUTIMBA
Yupo mwalimu, alimpiga mimba mwanafunzi akiwa form 3, wazazi walimlazimisha amuoe na mpaka sasa alimuoa na hakuna hatua ya kisheria iliyochukuliwa kwa mwalimu huyo.
MKUU WA SHULE ALIYEAMIA MKOLANI SEKONDARI ANAJUA HAYA.
Aliwahi kumshuhudia mwalimu wa kiume amemkumbatia mwanafunzi maabara kimapenzi ila hakufanya lolote.
KIKAO CHA WAZAZI JANUARI
Mkuu wa shule mpya aliitisha kikao januari, suala la uzinzi wa walimu lilisemwa, ila hakuna hatua stahiki zilizo chukuliwa.
Wenye mamlaka nendeni karejee minutes za kikao cha Januari cha wazazi mtajua.
WAZIRI WA ELIMU NA TAASISI HUSIKA
Hili limezidi, linawakwaza waalimu, sana sana wa kike. Kwasababu hakuna hatua stahiki zinazo chukuliwa.
Mkishindwa kazi zenu, tutawasaidia. Haiwezekani mabinti wanyanyaswe kingono wapumbavu nyie mpo.
Imagine anafanyiwa mwanao, utajisikiaje?
USHAURI
Ni kazi rahisi, TAKUKURU, wekeni mtego, mtawashika hawa wapumbavu wote asubuhi na mapema. Kuanzia mkuu wa shule anayelea mpaka hao walimu wanaoacha wake zao na kutafuna watoto.
Nawasilisha.