DOKEZO Walimu wa Shule ya Sekondari Rasesa wawashikisha watoto Pedi chafu

DOKEZO Walimu wa Shule ya Sekondari Rasesa wawashikisha watoto Pedi chafu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Gily Gru

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
8,632
Reaction score
23,673
Wasalaam

Jana jioni nimesikia kisa cha kushangaza sana. Wakati nikiwa kwenye simu naongea na aunt, mtoto wa form one (mtoto wa aunt) alirudi analia. Kumuliza analia nini? Akajibu shuleni wameshikishwa pedi chafu

Kisa kenyewe ni hiki kilichotokea shule ya Rasesa Secondary School huko Rawia Marangu
Choo cha shule kiliziba, na hii inatokana na watoto wa kike kutupa pedi chooni. Walimu walikerwa na hili sana sana

Muhusika wa kauzibua choo aliitoa ile pedi ikawekwa kwenye ndoo. Watoto wote wa kike kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne wakaitwa kwa majina hadharani.

Waalimu wakaamrisha kila mtoto wa kike ashike ile pedi iliyopo kwenye ndoo na mkono wa kulia kama adhabu siku nyingine wasirudie kutupa chooni.

Nimemshauri mama mdogo alifikoshe holi swala kwa afisa wa elimu.

Afisa Elimu Mkoa wa Kilimanjaro, Paulina Mkwama:
“Mmeshatupa taarifa ili turekebishe, mmefanya kazi nzuri, kumtuma tu Afisa Elimu Wilaya ni hatua, tunashukuru kwa kutuonesha lakini kilichobaki tutashughulikia sisi.

"Kazi yenu ni kutoa taarifa kama hivyo, mkituambia tu tunafanyia kazi ndio maana nikamtuma D.O akafanyie kazi.

"Ulivyoniuliza nilimjulisha RAS (Katibu Tarafa), Mkurugenzi na Afisa Elimu Wilaya, hivyo kama unataka kujua kilichoendelea baada ya hapo muulize source wenu aliyewapa hiyo taarifa."
 
Serikali inatakiwa iwapime walimu akili kama ziko sawa. Hawa walimu tunawqachia malezi ya watoto badala ya kujenga watoto wakawaharibu

Juzi hapo nilitoka kumwashia moto mwalimu mmoja wa darasa la tano. Aliwatuma watoto walete miti shuleni (ipandwe shuleni), sasa mtoto (related to me) akapeleka ua. Yule mwalimu alimtandika sana mtoto wa darasa la tano kwa kosa la kuleta ua na sio mti

Mtoto kurdish kulalamika kesho nikaamkia saa kumi na mbili kuhoji kwa nini amchape mtoto kwa kukosea kuleta ua baadala ya mti?

Akajiby mbovu, nusu nimkate makofi kama wasingeingilia walimu wengine kati. Nikamwita mwalimu mkuu kumhoji pia.

Nikamweleza kuwa kama mtoto kakosea kuleta mti kwa nini hakunfundisha? Kwa sababu watoto wengi wa mjini hawajui tofauti ya miti na maua.

Nikataka kuitisha shule nzima watoto huku nimeshika mhindi wautambue. Nikamweleza mwalimu mkuu nina uhakika nusu ya shule hawatatambua kama huu ni mhindi. Kama anabisha awaited watoto watambue.

Mwalimu mkuu akasema kweli sina haja ya kuita shule nzima watoto waliokulia mjini hawajui miti kama watoto wa vijijini. Mwalimu alikosea kumchapa mtoto angemfundisha

Yule mwalimu ni mpumbavu sana.
 
Wasalaam

Jana jioni nimesikia kisa cha kushangaza sana. Wakati nikiwa kwenye simu naongea na aunt, mtoto wa form one (mtoto wa aunt) alirudi analia. Kumuliza analia nini? Akajibu shuleni wameshikishwa pedi chafu

Kisa kenyewe ni hiki kilichotokea shule ya Rasesa Secondary School huko Rawia Marangu
Choo cha shule kiliziba, na hii inatokana na watoto wa kike kutupa pedi chooni. Walimu walikerwa na hili sana sana

Muhusika wa kauzibua choo aliitoa ile pedi ikawekwa kwenye ndoo. Watoto wote wa kike kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne wakaitwa kwa majina hadharani.

Waalimu wakaamrisha kila mtoto wa kike ashike ile pedi iliyopo kwenye ndoo na mkono wa kulia kama adhabu siku nyingine wasirudie kutupa chooni.

Nimemshauri mama mdogo alifikoshe holi swala kwa afisa wa elimu.
USIOE KAMA SIO BIKRA
 
Leo naomba niwatetee Waalimu maana mnawaandama sana.
Hayo ndo maisha ya Shule za Tanzania, mpaka ma Raisi waliokoteshwa Takataka shuleni, walifagia madarasa na Kudeki vyoo na hujawahi kusikia wamelalamika maana wanajua bila maarifa Yale wasingekua na nidhamu ya kuwafikisha hapo walipo.

Sasa watoto wamejaza pedi chooni ulikua unataka nani awajibike kuzitoa??, nani anaemjua alieiweka??, wangeadhibiwa Kwa viboko wakaumizwa si ungekuja na Uzi mwingine hapa kwamba mwanao kaonewa??
Unajua mziki wa kukaa na watoto 1200 kutoka familia tofauti Mkuu, Kila mtoto ana Kuja na tabia yake kutoka nyumbani kwao na unatakiwa uwasimamie wote wawe sawa, hiyo kazi ungepewa wew unafkiri ungekua hautelezi kwenye maamuzi yako as a human??
Plus, wazazi wenyewe mnaolea ndo kama wew Mkuu elimu haijakusaidia, mgomvi na mtu usiejua kutumia busara unafkiri hao walimu watakua na uzito kiasi gani wa kazi ya kumfundisha mwanao kitaaluma na malezi sahihi ambayo hayapati maskani??
Wanaweza wasiwe sahihi kwenye hilo lakini kabla hujawaanika hapa hebu vaa Viatu vyao kwanza...
 
Acha upumbavu, ulitaka walimu wao ndio washike na kuondoa hizo pedi chafu?
Watoto wa siku hizi hawasikii kabisa, walimu wapongezwe.
Tena wakirudia upuuzi wa kuchafua vyoo kwa kutupa pedi chooni hizo pedi wazibebe hadi vitandani mwao ndio akili itawakaa vizuri.

Walimu karibuni Marangu mtoni mnywe bia na kula nyama bili yangu nalipa.
 
Nimegundua humu ndani kuna matahira kabisa sio kuwa tu wana ugonjwa wa akili.

Hivi Leo utoe chooni pedi mbichi ina damu umshikishe mtoto kwa mikono yake mwenyewe iwe ni adhabu?

Ama kweli nilidhani nimeona mengi duniani.
 
Back
Top Bottom