Leo naomba niwatetee Waalimu maana mnawaandama sana.
Hayo ndo maisha ya Shule za Tanzania, mpaka ma Raisi waliokoteshwa Takataka shuleni, walifagia madarasa na Kudeki vyoo na hujawahi kusikia wamelalamika maana wanajua bila maarifa Yale wasingekua na nidhamu ya kuwafikisha hapo walipo.
Sasa watoto wamejaza pedi chooni ulikua unataka nani awajibike kuzitoa??, nani anaemjua alieiweka??, wangeadhibiwa Kwa viboko wakaumizwa si ungekuja na Uzi mwingine hapa kwamba mwanao kaonewa??
Unajua mziki wa kukaa na watoto 1200 kutoka familia tofauti Mkuu, Kila mtoto ana Kuja na tabia yake kutoka nyumbani kwao na unatakiwa uwasimamie wote wawe sawa, hiyo kazi ungepewa wew unafkiri ungekua hautelezi kwenye maamuzi yako as a human??
Plus, wazazi wenyewe mnaolea ndo kama wew Mkuu elimu haijakusaidia, mgomvi na mtu usiejua kutumia busara unafkiri hao walimu watakua na uzito kiasi gani wa kazi ya kumfundisha mwanao kitaaluma na malezi sahihi ambayo hayapati maskani??
Wanaweza wasiwe sahihi kwenye hilo lakini kabla hujawaanika hapa hebu vaa Viatu vyao kwanza...