Hao walimu mnawaonea bure. Kwa nini mtoa mada usishauri miundombinu mf sehemu ya kuchomea taka ijengwe kama haipo au wanafunzi waelimishwe madhara utupaji horera ya ped iliyotumika.
Tujiulize pia kuwa, mwalimu afanye nini kama sehemu sahihi ya kuweka hizo ped chafu ipo na wanafunzi kwa makusudi wanatupa huo uchafu sehemu isivyostahili?
Kama ulisoma shule za bweni tena za serikali, utakuwa unaelewa usumbufu wa wanafunzi unaofanywa kwa makusudi ili kuwakomoa walimu au kujitafutia umaarufu.
Tusikose fadhila kwa walimu kwa kukosoa na kubeza kazi nzuri wanazofanya licha ya kuandamwa na changamoto lukuki za kimaisha.